Karibu Kwenye Mtandao Wa Amsha Uwezo.
AMSHA UWEZO ni mtandao unaolenga kuhakikisha mtu anatumia kikamilifu nguvu kubwa iliyolala ndani yake ili kuishi maisha yenye uhuru. Kupitia huduma hii, unapata nafasi ya kutumia hazina kubwa ya uwezo mkubwa ulipo ndani yako kufanya mambo makubwa huku ukiendelea kuifanya dunia eneo zuri la kuishi.
Huduma ya AmshaUwezo imejikita katika maeneo matano ambayo kupitia haya mtu atafanikiwa kuamsha hazina hiyo kubwa ya uwezo wake kufanya makubwa na kufikia mafanikio makubwa. Maeneo hayo ni yafuatayo;
KUSUDI
Hakuna mwanadamu aliyezaliwa kwa bahati mbaya. Mwanadamu yoyote aliyefanikiwa kuja hapa duniani ana sababu maalumu ya kuiishi. Lakini watu wengi wameishi maisha mengine ambayo yapo nje ya kusudi lao la kuwepo hapa duniani. Mtu anapofanikiwa kutambua kusudi lake na kuanza kuliishi ndipo anapolazimika kuanza kuamsha hazina ya uwezo wake ili kuweza kulitimiza kusudi hilo. AmshaUwezo imejikita kuhakikisha kila mtu anatambua kwanza kusudi lake na hivyo kulazimika kuanza kuamsha uwezo wake.
NDOTO
Kila mwanadamu anayejitendea haki lazima awe na picha ya maisha fulani ambayo anatamani kuiona ikitimia kabla ya hajafa. Hii inakuwa dira ya wapi mtu huyo anataka aelekee. Ndoto ni jambo kubwa ambalo linaweza kuwashitua watu wengine unapowaambia lakini ni wewe pekee unayekuwa na imani kubwa kuwa inawezekana. Mtandao wa AmshaUwezo unahakikisha kila mwanadamu ambaye bado yupo hai anajenga ndoto ambayo ataiamini na kuwekeza kila alichonacho ili kuifikia. Kwa kufanya hivyo utaweza kuacha alama kubwa sana hapa duniani na kuendelea kuishi hata ukifa.
MALENGO
Kuwa na ndoto bila malengo ya kutimizia ndoto yako, ndoto hizo zinabaki kuwa matamanio tu. AmshaUwezo inahakikisha mtu anaweka malengo bora kisha mipango ya kupata matokeo ya ndoto yake. Kwa sababu ndoto zinachukua muda mrefu kutimia, AmshaUwezo inamwezesha mtu kuweka malengo ya muda mrefu na mfupi ya kumsaidia kutimiza ndoto yake.
HAMASA
Safari ya kuishi kusudi na ndoto ni ngumu inayohitaji hamasa ya kila wakati ili kusonga mbele. AmshaUwezo imejikita kuhakikisha mtu anakuwa na ari ya kuchukua hatua wakati wote bila kujali magumu anayoyapitia. Hamasa hii inajengwa kupitia dondoo, makala, semina, shuhuda nk ambazo zinatolewa mara kwa mara ili kuendelea kuchochea moto ambao umewasha ndani ya mtu. Hamasa huendelea kulipua mafuta ya uwezo ndani ya mtu ili kuendelea na kufika safari ya mafanikio makubwa.
USTAHIMILIVU
Kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako ni vita kubwa dhidi yako mwenyewe na dunia. Kuna ukinzani mkubwa na magumu ambayo mtu anaweza kukutana nayo. Katika hali hizo za magumu inakuwa ni rahisi mtu kukata tamaa na kuishi maisha yoyote anayokutana nayo. Mtandao wa AmshaUwezo unatambua hilo na hivyo kumpa mbinu za kujenga ustahimilivu wa kuendelea kuishi kusudi na ndoto zake licha ya magumu anayokutana nayo.
HUDUMA ZA AMSHA UWEZO
Mtandao wa AmshaUwezo umejikita kutoa huduma mbalimbali ili kukuwezesha kuchukua hatua za kuamsha uwezo wako na kuutumia kupata matokeo makubwa unayostahili. Huduma hizo ni kama ifuatavyo;
Makala na Dondoo
Hizi ni huduma ambazo zinatolewa kila siku kwenye blog, ukurasa wa facebook, wasap na instagram. Huduma hii inalenga kumfundisha na kumhamasisha mtu kuchukua hatua kila siku. Huduma hizi zinatolewa bure kabisa.
Vitabu
Mtandao wa AmshaUwezo una vitabu ambavyo vimesheheni maarifa na miongozo ya mtu kujua kusudi lake, kutengeneza ndoto yake halisi, kuweka malengo na kuyatimiza. Pia vina maarifa mengine ya kumwezesha mtu kuamsha uwezo wake na kufikia mafanikio yake makubwa anayostahili. Vitabu hivyo vinapatikana kwa gharama tofauti.
Ushauri
Mtandaao wa AmshaUwezo unataoa ushauri kwa wahitaji pale wanapokuwa njiapanda na kutokujua kwa kuelekea, au pale mtu anapokuwa kwenye njia ambayo hana uhakika kama itamfikisha unakotarajia kufika. Gharama za ushauri zinatofautiana kulingana na mkwamo alio nao mtu.
Mafunzo mabalimbali
Mtandao wa AmshaUwezo unatoa mafunzo mbalimbali yanayohusu kuamsha uwezo wa mtu na kufika mafanikio makubwa pale yanapohitajika. Mafunzo haya yanaweza kufanyika kwa njia ya semina za mtandao au ana kwa ana, kundi la wasap na mafunzo mengine kulingana na uhitaji. Gharama za mafunzo haya zinatofautiana kulingana na aina ya mafunzo.
Ukocha
Kuna kipindi katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa unahitaji usimamizi wa karibu ili uweze kupiga hatua. AmshaUwezo inakupa usimamizi wa karibu kwa kipindi kirefu ili kuhakikisha unapiga hatua kubwa ambazo zimeshindikana kwa kufanya pekeyako. Katika huduma hii, mimi Kocha nafanya kazi kwa karibu sana kwa kila hatua kukukwamua hapo uliponasa siku nyingi na kupiga hatua kubwa. Gharama za ukocha zinalipwa kulingana na miezi inayotumika kwenye ukocha.