Pata Mwongozo Wa Kuweka Na Kutimiza Malengo Yako
Umekuwa ni utamaduni wa kila mtu mwenye kiu ya kupata mafanikio kuweka malengo ili aweze kufikia kile anachokitamani. Mwanzoni mwa mwaka ndiyo muda ambao watu wengi huwa moto sana kuweka malengo ya kutimiza katika mwaka huo. Lakini hamasa hiyo huwa kama ukuni unaowaka peke yake ambao ni ndani ya muda mfupi tu hufifia na kisha kuzima kabisa. Kadri muda unavyoenda, malengo ya watu wengi huanza kusahaulika na baadaye kupotea kabisa hata kabla ya nusu ya mwaka kupita tangu wayapange malengo hayo.
Ni idadi ndogo sana ya watu wanaoweka malengo hufanikiwa kuyatekeleza na kupata matokeo yale waliyotarajia. Idadi kubwa ya watu wameendelea kuweka malengo kila mwaka bila ya kufanya utekelezaji unaoeleweka. Kwa kuwa malengo ndiyo dira ya mafanikio, watu wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao kwa sababu ya kutokuyaishi malengo yao.
Inawezekana umejiuliza mara nyingi, lakini hupati majibu ni kwa nini kila mwaka unaweka malengo lakini huyatimizi? Au kwa nini unapata matokeo madogo sana? Hakuna mchawi wa mbali anayesababisha hayo yote, mchawi ni wewe mwenyewe. Leo naenda kukupatia tiba ya tatizo hili. Lakini kabla sijakupatia dawa hiyo ambayo itaenda kutibu ugonjwa wako wa miaka mingi wa kuweka na kutotimiza malengo, naenda kukushirikisha sababu nne kubwa zinazochangia wewe kushindwa kuweka malengo na kutimiza na hivyo kuendelea kuishi maisha ya chini usiyostahili.
Sababu ya kwanza, Kutoweka malengo yenye ubora. Ni malengo yenye sifa bora ndiyo yanayoweza kutekelezeka na kupata matokeo makubwa unayotarajia. Watu wengi wamekuwa wakiweka malengo, lakini yamekuwa bora malengo na siyo malengo bora. Kwa kuwa natamani ufanikiwe nitakuambaia sifa za malengo bora na utaenda kuweka malengo yenye sifa hizo.
Sababu ya pili, Kutaka kumla ng’ombe mzima kama alivyo. Ukiambiwa ule ng’ombe mzima kama alivyo, utakata tamaa na kuona ni jambo ambalo haliwezekani. Lakini ng’ombe huyohuyo akikatwa vipande, utashangaa utakavyopata hamasa ya kula vipande vidogo vidogo mpaka unammaliza. Umeshindwa kutimiza malengo yako kwa sababu ya kung’ang’ania kutimiza lengo likiwa zima hivyo hivyo.
Sababu ya tatu, Kutoyaishi malengo yako. Kuweka malengo ni jambo moja tena la msingi, lakini huwezi kupata matokeo bila kuweka kazi. Unaweka kazi kwa kuyaishi malengo yako kikamilifu. Kuyaishi malengo ni kuchukua hatua kila siku na kupata matokeo madogo ambayo yakikusanywa yanaleta matokeo makubwa. Watu wengi wamekuwa mashuhuri wa kuweka malengo lakini hawachukui hatua za kuyatimiza. Hii imekuwa sababu mojawapo ya kutopiga hatua kubwa za mafanikio.
Sababu ya nne, Kutokujifanyia tathmini. Baada ya kuweka malengo, watu wengi wamekuwa wakiendelea kufanyia kazi tu malengo hayo bila kujua ufanisi wa hatua wanazochukua. Je upi mwenendo wako wa utekelezaji wa malengo yako? Changamoto gani zinajirudia katika utekelezaji wa malengo yako? Kwa mwenendo unaoenda nao utafanikiwa kutimiza malengo kwa wakati? Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza kila wakati katika safari yako ya kutimiza malengo. Kwa sababu umekuwa hujifanyii tathmini, muda mwingi umepotea na umeishia kupiga hatua ndogo za malengo yako.
Ndugu! Baada ya kutambua changamoto hii kubwa inayokukwamisha kupiga hatua kubwa kufikia mafanikio yako makubwa, nimekuandalia MWONGOZO WA KUWEKA NA KUTIMIZA MALENGO YAKO. Kupitia mwongozo huu utajua hatua za kuchukua ili kuweka malengo yenye sifa bora za kukufikisha kwenye mafanikio makubwa, hatua za kugawa malengo makubwa kwenye vipande na kuweza kutatimiza kirahisi. Si hivyo tu bali mwongozo unaeleza pia hatua za kuchukua ili kuyaishi malengo yako na kuyafikia kisha namna ya kujifanyia tathmini kujua ni kwa kiasi gani unapiga hatua za kutimiza malengo yako.
Mwongozo huu unaupata bure kabisa bila malipo yoyote. Hii ni zawadi yangu kwako ya kukufanya kupiga hatua na kufikia mafanikio unayoyatamani. Kupata mwongozo huu bonyeza kiunganishi hiki (https://www.amshauwezo.co.tz/mwongozowamalengo) kisha fuata maelekezo rahisi ya kuupakua na pia kutumiwa moja kwa moja kwenye email yako.
Si hivyo tu, bali baada ya kuupata mwongozo utaunganisha moja kwa moja kwenye mtandao wa AmshaUwezo ambapo utaendelea kujifunza zaidi na kupata hamasa za kuchukua hatua zaidi kupitia makala za kila siku na huduma nyingine. Usikose Zawadi hii muhimu ya maisha yako ya mafanikio. Kupata mwongozo bonyeza https://www.amshauwezo.co.tz/mwongozowamalengo
Asante.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz