Tumia Siri Hii Kuamsha Uwezo Wako Na Kutimiza Malengo Yako.
Punje ya mhindi ikiwa tu juu ya ardhi si rahisi kuipa thamani inayostahili. Unaweza ukapita na kuikanyaga na ikapasuka. Pia ndege wanaweza wakapita na kuila na historia yake ikaishia hapo.
Lakini kwa mkulima mwaminifu akiiona punje hiyo kamili huiona thamani kubwa sana ndani yake. Kwanza huiona punje hiyo kama mhindi ukiwa shambani ukiwa umebeba punje nyingine nyingi. Kisha huona shamba kubwa lenye mahindi likiwa limetokana na punje moja tu ya mhindi.
Hii inamaanisha kuwa punje ya mhindi inabeba uwezo ndani yake ambao ukiamshwa unazalisha vitu vya thamani kubwa sana. Kuna uwezekano wa kuzalisha idadi kubwa sana ya magunia ya mahindi kutoka kwenye punje hiyo moja. Lakini punje hiyo itafanikiwa kutoa thamani hiyo kama uwezo wake utaamshwa kwa kutengenezwa mazingira mazuri kama udongo, maji, mwanga na virutubisho.
Hivi ndivyo ilivyo kwa binadamu. Ndani yako una uwezo mkubwa na wa kipekee wa kufanya mambo makubwa yenye thamani kubwa. Uwezo huo umelala tu ndani yako. Hata wewe ambaye umekuwa ukilalamika kuwa maisha ni magumu unao uwezo huo. Sema tu hujauamsha ili ukufanyie kazi.
Kama punje ya mhindi inavyosubiri mazingira mazuri ili iote, ikue izae na kuzalisha, ndivyo ilivyo kwenye uwezo wako. Uwezo wako utaendelea kulala mpaka pale utakapochukua hatua za kuuamsha. Ndiyo maana umekuwa ukitamani kupata kitu fulani, lakini hupati. Umekuwa ukiweka malengo kila mwaka lakini utimizaji wake umekuwa hamna kabisa au hafifu sana. Sababu kubwa ya haya yote ni kutokuupa uwezo wako mazingira ya kuamka na kubaki macho mpaka utakapopata matokeo.
Mazingira mazuri ya uwezo wako si udongo, maji, mwanga au virutubisho kama ilivyo kwa punje muhindi bali ni tabia. Kuna tabia unazotakiwa kuzijenga na kuzilinda ili uwezo wako uamke na kukupa chochote unachotaka. Zifuatazo ni tabia zinazoweza kuamsha uwezo wako kukusaidia kupiga hatua;
Kujua kwa wazi kabisa unachokitaka. Uwezo wako utaamshwa kama kutakuwa kuna kitu kilicho wazi kabisa unachotaka. Ukijua nini hasa unakitaka maishani, utaamsha kiu kubwa kukipata na nguvu za kukipata zilizokuwa hazijatumika. Je unataka kuwa kiongozi mkubwa duniani? Je unataka kuwa mfanyabiashara maarufu wa nini? Je unataka kuwa mwanamuziki mkubwa Afrika?
Kuweka malengo. Huwezi kupata unachokitaka bila kujiwekea utaratibu wa kukipata. Utaratibu huo ni kuwa na tabia ya kuweka malengo. Ili uweze kutimiza malengo, lazima uamshe nguvu ya kukusaidia kupata matokeo. Kadri malengo yako yanavyokuwa bora ndivyo unavyokuwa kwenye nafasi nzuri ya kuamsha uwezo wako halisi.
Uvumilivu. Kwa sababu safari ya mafanikio makubwa huwa ni ndefu na yenye changamoto nyingi, huna budi kujijengea tabia ya uvumilivu ili kuendelea kutumia nguvu za kipekee ulizonazo hata pale unapokutana na magumu.
Ndugu! Nafahamu umekuwa ukiweka malengo kila mwaka kwa hamasa na furaha, lakini ukifika mwisho wa mwaka umekuwa ukiambulia patupu. Hii si kwa sababu huna uwezo ndani yako bali hujaziishi tabia ambazo zingeweza kuamsha uwezo wako kwa mwaka mzima na kupata mafanikio makubwa kadri mwaka unavyoenda.
Kwa kutambua hilo nimekuandalia semina ya siku kumi ambapo kwa kushiriki kwako utajifunza namna ya kuishi tabia nilizoanishwa hapo juu na nyingine nyingi ambazo zitaufanya mwaka huu 2022 na inayofuata kuwa ya kipekee kwako.
Mada ya semina hii ni: JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU MALENGO YAKO .
Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.
Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.
Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.
Asante kwa kujali,
Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz