Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuunguza Changamoto Zako Na Kupata Kile Ulichokitafuta Kwa Muda Mrefu Bila Mafanikio.


Categories :

Je wajua kuwa jua ndiyo chanzo kikuu cha nguvu hapa duniani? Nguvu unazozitumia kutembea zimetoka kwenye vyakula unavyokula ambavyo vimetokana na mimea ambayo nayo imepata nguvu kutoka kwenye jua. Kuni unazotumia kuivishia chakula au tofali zina nguvu ambazo zinatokana na jua. Kumbe siku jua likigoma kuwaka utakuwa mwisho wetu!

Licha ya jua kuwa na nguvu kubwa kiasi hicho lakini hujawahi kuiona karatasi au majani hata yale yaliyokauka yakiungua eti kwa sababu miale ya jua imetua juu yake. Hii ingekuwa hatari kubwa kwa maisha ya viumbe pia. Lakini kuna mazingira ambayo miale ya jua inaweza kufanya maajabu ambayo hujawahi kushuhudia. Ukichukua lensi mbinuko na kuielekeza kwenye jani kavu bila ya kuikwepesha, baada ya sekunde kadhaa jani hilo litaanza kuonyesha dalili za kuungua na baadaye kuwaka moto, huu sio uchawi! Haya ni maajabu ambayo unaweza kujifunza na kutumia kuunguza changamoto zako zilizokukwamisha kupata ulichokitafuta kwa muda mrefu.

Lensi mbinuko ina tabia ya kukusanya miale ya jua iliyotawanyika na kuielekeza sehemu moja. Miale hii ya jua iliyokusanywa pamoja ina uwezo mkubwa wa kuunguza jani hilo. Nguvu hii imekusanywa kutoka kwenye uelekeo tofauti tofauti na kuwekwa pamoja. Kuna somo kubwa sana la kujifunza kutoka kwenye maajabu haya. Ni miaka mingi sana umekuwa ‘busy’ kusaka mafanikio lakini bado hujapata mafanikio ya maana maishani mwako.

Miaka mingi uliyohangaika bila kupata mafanikio makubwa ni sawa na kawaida ya miale ya jua ambayo imekuwa ikielekea kwenye uso wa dunia kwa miaka mingi bila kushuhudia ikiunguza majani. Lakini pale miale michache ilipokusanywa pamoja na kuunganisha nguvu pamoja imetengeneza matokeo ya ajabu sana.  Hivi ndivyo inabidi ufanye kwenye maisha yako.

Hujafanikiwa kupata mafanikio makubwa ya kushangaza kwa sababu licha ya nguvu kubwa ulizonazo, umekuwa ukizitawanya sana na hivyo kukosa kukupa matokeo makubwa. Kwa kuamua kufanya mambo mengi sana kwa wakati mmoja, umetawanya nguvu zako na hivyo kukosa madhara. Kila fursa ikija kwako umeona inakufaa na ndiyo maana umeanzisha biashara nyingi sana, na mpaka sasa nyingi zimekufa hata kabla ya kukupa faida inayoeleweka. Umeamka asubuhi bila kujua unaenda kufanya nini, ndiyo maana umekuwa ukifanya chochote kinachokujia. Kuna mabadiliko makubwa sana yatatokea pale utakapoamua kukusanya nguvu zako.

Malengo . Moja ya lensi unayoweza kutumia kukusanya nguvu zako ni kuwa na malengo. Sifa ya malengo bora ni kukusanya nguvu zako na kuelekeza sehemu moja au chache ambako ukikaa huko kwa muda mrefu utafanikiwa kupata matokeo makubwa. Ukiwa na malengo utaanza mwaka, mwezi, juma au siku ukijua wapi unaelekea.

Malengo yanachoma changamoto. Kama miale ya jua ilivyo na uwezo wa kuunguza jani pale inapodondoka kwenye jani hilo na kuzuiliwa kupita, ndivyo ilivyo kwenye malengo. Mtu anapoelekeza nguvu na umakini wake kwenye jambo moja kwa muda mrefu changamoto hiyo inaungua na kufanikiwa kupita na kupata kile unachokitafuta.

Ndugu hii ni tiba nzuri sana ya kupata chochote unachotaka. Kwa kuzingatia umuhimu wa tiba hii nzuri ya mafanikio yako mtandao wa AmshaUwezo umekuandalia semina ya siku kumi yenye mada JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO.  Miongoni mwa masomo yatakayofundishwa ni MALENGO. Kwenye somo hili utafundishwa namna ya kuweka malengo na jinsi unavyoweza kutumia malengo hayo kama lensi ya kukusanya nguvu na kuunguza changamoto kisha kupata mafanikio uliyoyakosa kwa miaka mingi.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz  
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *