Hivi Ndivyo Ulivyofanikiwa Kutelekeza Malengo Yako


Categories :

Mwaka ulipoanza ulikuwa miongoni mwa watu walioanza mwaka kwa hamasa kubwa. Hamasa hii ilikuja baada ya kuona watu wengi wakiongelea kuhusu malengo. Mwaka mpya na mambo mapya! Ulipiga picha na kuona mpaka mwaka unaisha utakuwa umeshafika mbali sana kwa kuyapata matokeo uliyotarajia.

Je ukijiuliza leo ni hatua gani umeshazipiga tangu ulivyoyaweka malengo yako? Ni zaidi ya mwezi mmoja na nusu tangu mwaka 2022 uanze, una chochote mikononi? Au na wewe ni miongoni mwa watu ambao kadri siku, majuma  na miezi ilivyozidi kwenda umekuwa unasahau malengo yako? Watu wengi wameshasahau malengo yao, au wanayakumbuka kwa kiasi kidogo sana.

Moja ya sababu zilizokufanya kuanza kuyasahau au kuyasahau kabisa malengo yako ni kutoyawekea mipango  ya utekelezaji. Baada ya kujua malengo yako na kuyapanga, hatua inayofuata ni kuingia kwenye utekelezaji. Hii ni sawa na kupanga safari, ukijua kwa dhati wapi unaelekea , baada ya hapo huwa unaweka mipango ya namna gani utaweza kufika kule unakotaka kwenda. Baada ya kuweka malengo yako, uliweka mipango gani ya kuhakikisha unakamilisha malengo yako? Kwa sababu hukuweka mipango thabiti ya hatua za kuchukua , ndiyo maana ulipoamka hukujua nini unaenda kukifanya ili uweze kukamilisha malengo yako. Pia ndiyo sababu iliyosababisha kuanza kupoteza taratibu hamasa yako.

Ili uweze kutimiza malengo uliyopanga, ni lazima ufahamu kwa wazi hatua utakazochukua ili kuweza kutimiza malengo yako. Kwa mfano kama lengo lako lilikuwa ni kuongeza kipato chako kwa 50% ambacho ni milioni tano (sh 5,000,000/) lazima uweke bayana kabisa ni kwa njia zipi utafanikiwa kuongeza kipato chako. Je utaongeza kiasi cha mauzo ya biashara yako kwa kutafuta wateja wapya? Je utapunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kupunguza gharama za uendeshaji? Kama lengo lako lilikuwa ni kuweka akiba ya shilingi milioni moja kwa mwaka, je umepanga kuweka asilimia ngapi kwenye kila kipato chochote unachopata?

Mipango yako unayoweka lazima itoe matokeo unayotarajia kuyapata. Matokeo tarajiwa ndiyo vitakuwa viashiria kuwa unatekeleza mipango yako na inafanikiwa. Ukifanikiwa kuanza kupata matokeo, utapata hamasa kubwa ya kuzidi kuchukua hatua. Malengo yako yasipokuwa na mipango thabiti yatakosa matokeo na hivyo kukosa hamasa ya utekelezaji. Hii ni sababu mojawapo iliyokufanya uanze kusahau au kusahau kabisa malengo yako.

Kaa chini leo na yapitie malengo yako kuona ni mpango gani uliyoliwekea kila lengo lako la mwako huu. Je ni kwa kiasi gani umeutekeleza mpango huo? Uwekaji na utimizaji wa malengo imekuwa changamoto kwa watu wengi na hivyo kuwa kikwazo kikubwa kwa watu kupiga hatua kubwa. Kwa kulitambua hilo na kukujali wewe ndugu yangu, mtandao wa AmshaUweza umekuandalia semina ya siku kumi ambayo itakusaidia kupitia malengo yako na mipango kukuwezesha kuyatimiza malengo yako ya mwaka 2022 na miaka mingine kwa ushindi mkubwa.

Mada ya semina hii ni  JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *