Kama Unataka Mafanikio Zaidi Ongeza Kitu Hiki Kwa Watu Wengine.


Categories :

Ndoto ya mafanikio makubwa imetawala vichwa vya watu wengi. Kila mtu anatamani kila wakati apige hatua chanya, atoke kutoka kwenye mafanikio madogo yasiyomridhisha na kwenda kwenye mafanikio makubwa ambayo ataridhika. Ndiyo maana kila siku watu wanaamka asubuhi na kuweka jitihada ili waweze kulifanikisha hilo.

Licha ya jitihada wanazoweka, lakini kupata matokeo ya kuwafikisha kwenye mafanikio hayo makubwa imekuwa changamoto kwa watu wengine. Kwa sababu ya kuweka juhudi kubwa na kukusa matokeo wanayotarajia, kuna watu wanakata tamaa na kuishia njiani. Lakini licha ya watu wengi kukosa matokeo tarajiwa, wapo watu waliofanikiwa kupiga hatua kubwa na kufikia mafanikio makubwa. Watu hawa wamedhaniwa kuwa ni wenye bahati fulani au wenye upekee fulani. Inawezekana na wewe umekuwa miongoni mwa watu ambao unawaonea wivu waliofanikiwa ukiamini wana bahati ya kipekee Fulani ambayo wewe huna.

Lakini watu hao waliofanikiwa, hawana bahati, na hata kama wanaipata basi ni pale bahati hiyo inapokutana na maandalizi. Siri kubwa wanayoijua watu hawa na ndiyo wanaoiishi na kupata mafanikio makubwa ni thamani kwa watu wengine. Wametambua ni kitu gani watu wanaowazunguka wanakihitaji, kisha wakawapa thamani hiyo watu hao zaidi ya matarajio yao.

Zig Ziglar alisema ‘’You can have everything in life you want, if you will just help other people get what they want’’ akimaanisha kuwa unaweza kupata chochote unachotaka maishani kama utawapa watu wengine kile wanachokitaka. Kumbe ili uweze kupata mafanikio makubwa maishani mwako lazima kwanza utambue ni thamani gani watu wanataka ili uwape thamani hiyo kwa kiwango kikubwa ambacho wataona kama wamependelewa. Imekuwa kasumba kwa watu wengi hata kwenye biashara ya bidhaa au huduma, kuja na biashara ndipo kuanza kutafuta wateja. Kumbe kinyume chake ilikuwa sahihi.

Inawezekana tayari una mafanikio ambayo umeshayapata lakini hayakuridhishi. Ili uweze kupata mafanikio makubwa unayostahili huna budi kuongeza thamani kwa watu wengine. Kadri unavyozidi kutoa thamani kwa watu wengine ndivyo unavyozidi kuwashawishi watu wengine kukupa kile unachokitaka. Umepata mafanikio madogo maishani mwako kwa sababu umetoa thamani ndogo kwa watu wengine.

Ili uweze kupata mafanikio makubwa zaidi mwaka huu, weka jitihada kubwa kwenye kuhakikisha unaongeza thamani kwa watu wengine. Kama unafanya biashara basi hakikisha unaongeza ubora wa huduma unayowapa wateja wako. Kadri utakavyoongeza ubora wa huduma ndipo utapata mauzo zaidi na faida zaidi. Kama unataka mafanikio zaidi kwenye mahusiano, hakikisha unaongeza thamani ya mahusiano yako ikiwemo muda bora, usikivu, kujali, misaada nk. Kwenye kila eneo la maisha yako ongeza thamani ili uweze kupata matokeo makubwa zaidi.

Kuhakikisha hilo linawezekana, mtandao wa AmshaUwezo umekuandalia semina ya siku kumi ambayo itakuwezesha kutambua mbinu utakazotumia kuongeza thamani kwa watu wengine ili uweze kupiga hatua kubwa kwenye malengo yako ya mwaka 2022 na miaka inayofuata ya maisha yako.

Mada ya semina hii ni  JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 machi, mpaka tarehe 10, machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/lvfrgvlqf3kdeh5klocvqc
kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

imeandaliwa na alfred mwanyika
kocha na mwalimu wa uwezo wako halisi
mawasiliano;
simu; 0752206899/0714301952
barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *