Nini Kilichobaki Baada Ya Kusahau Kile Ulichojifunza Shuleni?
Maisha yako huendeshwa na kile unachokifahamu. Unachokifahamu ndiyo kinakuwa mwongozo wa wewe ufanye nini. Mawazo anayoyawaza mtu pia hutegemea zaidi na kile kilichotawala fikra zake. Kadhalika maamuzi anayoyatoa mtu hutegemea na kile anachokifahamu kwa kuona kitaleta matokeo bora. Kumbe hatua za maisha ulizofikia ni matokeo ya kile unachokifahamu na kukitumia kukupa matokeo.
Ili kuweza kufahamu vitu, kumekuwa na mifumo ya elimu ambayo tangu utotoni mtu huanza shule na hukua akiwa shule mpaka anakuwa mtu mazima anayejitegemea. Mtu akiwa shuleni hutegemewa apate elimu ambayo itampa ufahamu wa kumwezesha kuishi maisha yake kwa mafanikio. Ndiyo maana kumekuwa na msisitizo mkubwa sana kuwa mtu uende shuleni, usome kwa bidii, upate ufaulu mkubwa kisha upate kazi nzuri. Baada ya hapo maisha yako yatakuwa ya mafanikio mazuri.
Kuna watu wengi sana waliofuata dhana hiyo, wameenda shule wamesoma kwa bidii na kupata ufaulu mzuri na kupata kazi nzuri. Lakini licha ya kupata kazi nzuri hawajaweza kupiga hatua kubwa sana katika maeneo mengi ya maisha yao. Sababu mojawapo ya kwa nini elimu ya shule pekee yake hazimhakikishii mtu kupata chochote anachotaka inaelezwa vizuri na kauli hii aliyoisema Albert Einstein kuwa “Education is what remains after one has forgotten what one has learned in school.” Akimaanisha kuwa elimu ni kile kinachobakia baada mtu kusahau yale aliyojifunza shuleni.
Kuna vitu vingi sana anavyojifunza mtu kipindi akiwa shuleni, Lakini ni vichache sana ambavyo huja kuvituma katika maisha nje ya shule. Kaa chini na tafakari ni kwa kiasi gani cha maarifa uliyoyapata shuleni unakikumbuka na unakitumia sasa? Hii inamaanisha kuwa ili uweze kupiga hatua kubwa zaidi katika maisha yako, unahitaji maarifa zaidi ya yale uliyoyapata shuleni. Kuhitimu shule hakupaswi kuwa mwisho wa maarifa bali mwanzo na mwendelezo wa kupata maarifa zaidi ya kukuwezesha kumudu maisha baada ya shule.
Jiulize swali hili leo, ni kiasi gani cha maarifa kilichobakia baada ya kusahau yale mengi uliyojifunza shuleni? Je huoni kama kuna pengo ambalo inabidi ulizibe ili uweze kupita kisha kuchukua hatua kubwa zaidi? Je huoni kuna elimu ya msingi kuhusu fedha unayohitaji ya namna ya kutengeneza thamani kisha watu kukulipa sawasawa na thamani unayoitengeneza? Je huoni kuna elimu kuhusu biashara unahitaji ili uweze kutengeneza biashara inayojiendesha na ambayo haikupi ukomo wa kiasi cha fedha unachoweza kuzalisha? Je huoni unahitaji uelewa kuhusu hazina kubwa ya uwezo uliyonayo ili uweze kuuamsha uwezo huo na kufanya mambo makubwa zaidi ya yale uliyoyapata kwa kufanya mazoea?
Ndugu ili uweze kuboresha maisha yako kwa kupiga hatua kubwa zaidi huna budi kuhakikisha kila wakati unapata maarifa sahihi kwa wakati sahihi. Kwa kuzingatia hilo mtandao wa AmshaUwezo umekuwa ukiwashirikisha watu maarifa mbalimbali ili waweze kuchukua hatua sahihi na kupata matokeo wanayostahili. Nafurahi kukutaarifu kuwa mtandao huu umeandaa semina ya siku kumi itakayokupa maarifa muhimu sana kuhusu uwezo wako na malengo yako ili uweze kuuishi mwaka 2022 na miaka inayofuata kwa mafanikio makubwa.
Mada ya semina hii ni JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.
Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.
Gharama za semina hii ni shilingi elfu tano tu (5,000/) kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.
Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/lvfrgvlqf3kdeh5klocvqc
kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.
Asante kwa kujali,
imeandaliwa na alfred mwanyika
kocha na mwalimu wa uwezo wako halisi
mawasiliano;
simu; 0752206899/0714301952
barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
tovuti: www.amshauwezo.co.tz