Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuiyeyusha Hofu Yako Na Kuendelea Na Safari.


Categories :

Hofu imekuwa ni ukuta mkubwa sana unaojengwa kati ya mtu na mafanikio yake. Watu wengi wameshindwa kuchukua hatua sahihi kwa sababu ya hofu kusimama mbele yao. Kwa sababu ya kikwazo hiki kikubwa cha mafanikio, watu wametamani hofu ingekuwa kiumbe hai, ili siku moja ife. Kwa bahati mbaya hofu ipo kila siku; jana, leo na kesho.

Hofu ni kitu cha kufikirika. Ndiyo maana huwezi kusema ulikutana na hofu mahali fulani ikipunga upepo. Kwa namna nyingine hofu ni kitu mtu anachokijenga kwenye fikra zake, ndiyo maana kwenye tukio hilo hilo moja, watu wawili wanaweza kuwa na viwango tofauti vya hofu. Moja ya hofu inayowakumba na kuwakwamisha watu wengi kupiga hatua ni hofu ya kushindwa. Hii ni hofu anayoijenga mtu baada ya kutarajia matokeo hasi au mabaya kwenye jambo analolitarajia.

Nenda tu, usiogope!

Kwa asili hakuna mtu ambaye hana hofu kwani kila mtu ana hofu, lakini tofauti inakuja kwenye namna ya kuikabili hofu. Tofauti mojawapo kati ya watu waliofanikiwa na wale walioshindwa ipo kwenye namna ya wanavyoikabili hofu. Waliofanikiwa wakikutana na hofu hawaikimbii au kugeuka na kurudi nyuma bali hujipa ujasiri wa kuchukua hatua kwenye uelekeo sahihi wa kupata matokeo bila kujali kuwa hofu ipo huko. Kuna mambo mengi ambayo umeshindwa kufanya baada ya kushikwa na kushindwa na hofu ya kushindwa. Lakini una uwezo wa kuikabili hofu na kufanikiwa kupiga hatua unazotarajia.

Ili uweze kuikabili hofu vizuri, kwanza huna budi kuifahamu hofu vizuri. Kama tulivyoona hapo juu kuwa hofu ni kitu cha kufikirika na cha kutengenezwa, hivyo mhusika mkuu wa kuikaribisha na kuikabili ni wewe. Kwa sababu hofu ya kushindwa inakuja pale unapokuwa huna uhakika wa kupata matokeo unayoyatarajia, njia mojawapo ya kuikabili ni kujiandaa vizuri. Unapotambua kuwa kuna kitu fulani kinaweza kikatokea ambacho si kizuri kwako, basi huna budi kuweka mazingira bora ili kuongeza uhakika wa kupata matokeo tarajiwa.

Licha ya maandalizi unayoweza kufanya, njia nyingine itakayokusaidia kuikabili hofu ya kushindwa ni kutambua kuwa hofu nyingi tunazozipokea huwa siyo halisi. Tafiti zinaonyesha kuwa vitu vingi tunavyovihofia havitokei, hata vikitokea sio kwa ukubwa ule ambao tuliufikiri. Jiulize mwenyewe ni mambo mangapi uliyahofia lakini matokeo yalikuwa tofauti kabisa na hofu uliyokuwa nayo? Ukihesabu utakuta ni matukio mengi sana ambayo uliyahofia lakini matokeo yalipotoka ilikuwa tofauti kabisa na matarajio.

Ndugu ukizingatia namna ambavyo hofu imekuwa kikwazo kwako huna budi kuwekeza nguvu kubwa kuhakikisha unapiga hatua unazozitarajia licha ya hofu hiyo kuwa mbele yako. Kuna hofu inayoweza kuwa imesimama kwenye malengo yako ya mwaka huu 2022. Hofu hiyo inaweza kuwa ni ileile iliyokukwamisha mwaka jana. Ufanye mwaka huu uwe wa kipekee kwako, itambue hofu kiundani na anza kukabiliana nayo kwa kuiendea bila kurudi nyuma.

Mtandao wa AmshaUwezo unatambua umuhimu wa kujua namna ya kukabiliana na hofu ya kushindwa hivyo umeandaa semina ya siku kumi ambapo moja ya somo litakalofundishwa kiundani ni namna ya kuikabili hofu ya kushindwa.  Hii itakuwa ni nguzo muhimu sana kwako ya kuhakikisha malengo yako ya mwaka huu na miaka mingine yanatimia.

Mada ya semina hii ni  JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni shilingi elfu tano tu (5,000/) kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/lvfrgvlqf3kdeh5klocvqc
kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha Na Mwalimu Wa Uwezo Wako Halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *