Siri Ya Mafanikio Iliyojificha Kwenye Kuamka Mapema.


Categories :

Moja ya nidhamu ambayo imekuwa changamoto kwa watu wengi ni kuwahi kuamka. Usingizi umekuwa mtamu kwa watu wengi kunapokaribia kucha na hivyo wengi kushindwa kuwahi kuamka. Inapofika saa kumi au saa kumi na moja alfajiri, watu ndiyo huvuta shuka vizuri ili waweze kumalizia usingizi wao.

Lakini moja ya tabia ambayo watu waliofanikiwa wamejijengea ni kuamka mapema. Watu hulala mapema ili waweze kuamka mapema pia. Wengi wao huamka kabla ya watu wengi hawajaamka. Inaelezwa kuwa kuwahi kuamka ni siri ya ufanisi mkubwa wa watu wengi waliofanikiwa. Kwa hiyo kama umekuwa ukipata mafanikio kiduchu inawezekana sababu mojawapo ni ufanisi mdogo unaosababishwa na kuchelewa kuamka alfajiri.

Kuna faida nyingi sana za kuwahi kuamka, ikiwemo kuimarisha ubora wa usingizi. Afya ya akili na ufanisi. Unaweza kujifunza faida hizi ili na wewe uweze kuzitumia katika kupiga hatua na kufikia mafanikio makubwa kama wale walikwisha kuyapata.

Kuamka mapema kunaboresha namna ya kufikiri. Tafiti zinaonyesha kuwa watu wanaowahi kuamka wana uwezo mzuri wa kubaki na kufikiri jambo moja (focus) na kuwa na nguvu siku nzima ukilinganisha na wale wanaochelewa kuamka. Pia watu hawa na uwezo wa kutatua matatizo haraka kuliko wale wanaochelewa kuamka. Kwa kuwa huwezi kutenganisha mafanikio na kufikiri bora huna budi kuboresha namna ya kufikiri kwa kuanza kuwahi kuamka.

Kuamka mapema kunakupa uhakika wa muda wa kufanya mazoezi. Huwezi kutenganisha afya njema ya mwili na mafanikio kwani ndiyo mtaji wa kwanza kabisa wa kufikia mafanikio yako. Moja ya hitaji muhimu kwa afya ya mwili ni mazoezi. Muda na nidhamu ya kufanya mazoezi kwa watu wengi imekuwa ni changamoto. Kuwahi kuamka kunakupa uhakika wa kufanya mazoezi kuliko jioni ambapo mwili unakuwa umeshachoka kwa ajili ya kazi za siku nzima.

Kuamka mapema kunakupa nafasi kubwa ya kutimiza malengo. Ukiwahi kuamka kunakupa fursa nzuri ya kuipangilia siku yako vizuri kuliko aliyechelewa kuamka. Kwa kayaandika malengo yako unayoenda kuyafanyia kazi inakujengea mtazamo wa kuiendea siku kwa ushindi zaidi kuliko ukichelewa kuamka na kuianza siku kwa ‘pressure’ pengine hata bila ya kuipangilia siku yako.

Kuamka mapema ni nidhamu muhimu sana katika kujenga mafanikio makubwa na ya kudumu. Waliofanikiwa waliifahamu siri hii na kuiishi. Kumbe na wewe unaweza kuijenga tabia hii na kuitumia ili kuanza kujenga mafanikio ya maisha yako. Inafahamika kuwa watu wengi wamejaribu hili lakini wakashindwa na kuishia njiani, lakini wewe usiwe miongoni mwao.

Kwa kutambua umuhimu wa siri hii ya kuwahi kuamka na kujenga tabia hiyo, mtandao wa AmshaUwezo umekuandalia semina ya siku kumi ambapo moja ya masomo yatakayofundishwa ni muujiza wa alfajiri. Kwa kujiunga na kushiriki semina hiyo utajifunza kiundani kuhusu siri hii ya kuwahi kuamka na pia kupata mbinu za kujenga tabia hii ili uweze kufaidika nayo.

Mada ya semina hii ni  JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni shilingi elfu tano tu (5,000/) kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/lvfrgvlqf3kdeh5klocvqc
kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

imeandaliwa na alfred mwanyika
kocha na mwalimu wa uwezo wako halisi
mawasiliano;
simu; 0752206899/0714301952
barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *