Usiyasikilizie Maumivu ya Sindano Bali Furahia Ilichokibeba.


Categories :



Mtu akienda hospitali kutibiwa, kudundwa sindano inaweza kukawa ndio njia pekee ya kupata matibabu. Mgonjwa akisikia habari ya kudundwa sindano mwili wake husisimka na huku hofu ikimtawala kwa sababu ya maumivu makali ya sindano ambayo anatarajia kuyapata.

Lakini maumivu hayo huweza kupungua pale anapoona maumivu aliyonayo yatapotea kwa kuvumilia maumivu hayo makali lakini ya muda mfupi. Maumivu hayo hupotea kwa thamani inayokuwa imebebwa na sindano ambayo ni dawa. Dawa hiyo ndiyo itakayokuponya na maumivu ya muda mrefu unayoyapata kwa sababu ya ugonjwa.



Maisha ya mafanikio makubwa huambatana na changamoto na vikwazo vyenye maumivu makali. Ni rahisi sana kuyakimbia maumivu hayo kama mgonjwa ambavyo angeweza kukimbia kama asingejua thamani iliyobebwa kwenye maumivu ya sindano.

Imekuwa ni rahisi sana kuyaona mafanikio kwa mtu na kutamani kuyapata kama yeye alivyopata. Lakini kuna kitu ambacho watu wanaoyatamani mafanikio huwa wanakuwa hawajakiona. Ni gharama za kuyapata mafanikio hayo wanayoyatamani. Hizi ni gharama zilizoambatana na maumivu makali, hivyo waliyapata mafanikio hayo baada ya kuwa radhi ya kuyavumilia maumivu hayo makali ili kupata kile kikubwa walichokitamani.

Ndugu! Maumivu ya mafanikio makubwa ni makali sana, hutakuwa radhi kuyavumilia kama hutajua ni kitu gani utakachofaidika nacho. Kumbe kitu cha kwanza unachotakiwa kukijua katika safari hii ni thawabu utakayopata baada ya kuvumilia mateso yote ya safari hiyo.

Thawabu utakayoipata lazima iwe kubwa kuliko mateso ambayo utakuwa unayakabili. Unapata nini baada ya mateso hayo? Kama utakuwa unayaiga tu kile watu wengine wanafanya, inakuwa si rahisi kwa wewe kuwa na sababu kubwa ambayo itakufanya ustahimili maumivu.

Kuwa na maono ambayo licha ya kuwa sindano lakini yatakuwa na thamani kubwa imebebwa ndani yake. Licha ya maumivu ambayo yatajitokeza lakini utaendelea kuyaishi kwani kila ukichungulia thamani yake utaona ni kubwa sana licha ya maumivu ayoyapata.

Chunguza umebeba nini ndani yako? Thamani gani umebeba kwa ajili yako na dunia? Je ni kuwatoa watu kwenye umasikini mnene? Je ni kuwaongozo watu ili wafikie ndoto zao? Je unaona thamani kubwa sana baada ya kuvuka hatua hiyo licha maumivu yaliyoambatana?

Tambua maono yako sasa, tengeneza thamani yake bayana, anza kuyaishi, ukikutana na maumivu nenda kaangalie thamani yake. Hii itakupa hamasa ya kuendelea.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *