Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwasha Moto Usiozimika Milele.
Harakati za kuishi na kupata mafanikio makubwa ni sawa na kuwasha moto usiozimika. Katika mazingira ya kawaida, ili uweze kuwasha moto wa kuni unahitaji kuni na kwa kuanza kuni ndogo ambazo zitashika moto kwa wepesi kisha uwepo wa kuni kubwa ili ziwake kwa muda mrefu.
Ili moto huo uendelee kuwepo lazima kuni ziendelee kuwepo na kuwaka. Hivyo kabla ya zile za mwanzo hazijateketea inakupasa kuweka kuni nyingine ili ziambukizwe moto za zile za awali. Ukiendelea kufanya hivyo hakuna namna ambayo moto huo utazima. Hivi ndivyo unavyotakiwa ufanye ili uweze kupata mafanikio makubwa na ya kudumu. Unahitaji kuwa na moto wa hamasa isiyoisha wala kupungua. Hamasa kwa ajili ya kuchukua hatua inabidi lisiwe tukio lakini maisha.
Watu wengi wameshindwa kupata mafanikio kwa sababu ya kuwa na hamasa za matukio. Kwa mfano akikutana na mtu aliyepiga hatua kubwa na kuwa na mafanikio yanayoonekana, atahamasika sana na kuona na yeye anaweza kufanya na kupata mafanikio aliyoyapata mtu huyo. Huondoka kwa hamasa kubwa kuwa anaenda kuweka kazi. Lakini wengine hamasa hiyo hupotea baada ya siku chache tu kupita hata kabla ya kuanza. Wengine hufanikiwa kuanza lakini hamasa hiyo huanza kupungua na baadaye kuisha baada ya kukutana na changamoto. Kadhalika mtu aliyehudhuria semina na kupata mafunzo, huhamasika na kuona sasa amepata njia ya kuelekea kupata mafanikio yake, lakini kadri siku zitakavyokuwa zinapita ndivyo hamasa hiyo huendelea kupungua na baadaye kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Kumbe ili upige hatua kubwa na kuyafikia mafanikio ya ndoto yako, huna budi kuhakikisha una hamasa ya kuchukua hatua muda wote. Hakikisha umetengeneza mazingira ya kuhakikisha gari la hamasa yako halizimi ili hata unapokutana na magumu unasonga mbele. Vifuatavyo vitakusaidia kuwasha moto wa hamasa usiozimika.
Kutambua kusudi lako; Hiki ndiyo kitu cha kwanza kabisa ambacho inabidi ufanye bidii kukipata. Kutambua kusudi lako ni kujua sababu ya wewe kuwepo hapa duniani. Una kitu gani maalumu ulicholetwa ukifanye? Kila mtu ana sababu ya pekee ya kuwepo hapa. Ukitambua sababu ya wewe kuwepo hapa na kuanza kuifanya itakufanya upate hamasa ya kuendelea kufanya hata pale utakapokutana na changamoto. hamasa hiyo itajengeka kwa kutambua kuwa upo hapa duniani kwa kazi hiyo tu na hakuna mtu mwingine anayeweza kuifanya kwa niaba yako.
Kuzungukwa na watu sahihi. Je watu ulio karibu nao wanachochea au kuzima kuni za hamasa? Au ndiyo wanazima moto unaowaka? Ili moto wa mafanikio usizime inabidi uzungukwe na watu ambao hata ukipatwa na changamoto wataendelea kukutia moyo kuwa uendelee na jitihada kwani utafanikiwa usipokata tamaa. Pia hata pale utakapokuwa unawaambia ndoto yako kubwa watakuambia una uwezo wa kuifikia.
Ili kuweza kutambua kusudi lako na kuzungukwa na watu sahihi, mtandao wa AMSHA UWEZO umeandaa kundi maalumu na la kudumu la wasap litakalo kusaidia kujenga hamasa ya kudumu na kisha kufanikiwa kuishi maisha ya mafanikio. Kwa kujiunga na kundi hilo utapata
1. Mafunzo mbalimbali kama semina
2. Usimamizi wa malengo yako
3. Miongozo kama Kutambua kusudi lako, kuweka na kutimiza malengo
4. Makala na dondoo kila siku
5. Hamasa, kwa kuwa karibu na watu sahihi
6. Uchambuzi wa vitabu
Ada ya kujiunga na kundi hili ni shilingi elfu kumi (10,000/) tu, ambayo unaweza kulipa kwa awamu mbili. Ada hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani kubwa utakayoipata, lakini lengo lake ni kuhakikisha huikosi nafasi hii muhimu maishani mwako kwa sababu ya gharama. Hii siyo ya kuikosa, chukua hatua leo.
Bonyeza kiunganishi hiki kujiunga
https://chat.whatsapp.com/Dx1HF02stFq2LxIqoRTAUD
Kwa maelezo zaidi piga 0752 206 899/0714 301 952 (Mwl. Alfred Mwanyika)
“Wekeza kwenye Maarifa Timiza Malengo Yako”