Kama Bado Upo Hai, Bado Hujachelewa.
Katika maisha yako kuna mtu wa aina fulani ulitamani uwe lakini mpaka sasa hujawa mtu huyo. Katika maisha yako kuna hali fulani ya kifedha ulitamani uifikie ili uwe huru, lakini hujaifikia licha jitihada unazoweka. Katika maisha yako kua maeneo fulani ya dunia ulitamani uyafikie kabla hujaiaga dunia, lakini mpaka sasa hujayafikia.
Kila binadamu, huwa anakuwa na matamanio ya kuwa mtu fulani katika maisha yake kama wewe ambavyo umekuwa ukitamani. Inawezekana umefika hatua ukakata tamaa kwa kuona sasa huwezi kuwa mtu yule uliyetamani kuwa. Baada ya kivuja jasho jingi bila matokeo umeaona kama hili halitaweza kutokea maishani mwako. Baada ya umri kwenda umeona kama sasa huwezi kuwa mtu wa aina uliyotamani kuwa. Hivyo umekata tamaa.
Lakini kama unaweza kusoma hapa, basi nina habari njema kwako kuwa; kama hujafa basi hujachelewa. Hata sasa unaweza kuwa mtu yeyote unayetaka kuwa, unaweza kwenda kokote na kupata chochote. Kitu pekee am acho kingeweza kukutenganisha na jinsi ulivyotaka kuwa ni kifo pekee.
Je upo kwenye njia sahihi? Ili uweze kuwa mtu wa matamanio yako lazima utembee kwenye njia yako sahihi ya hapa duniani. Kuwa mtu wa maisha yako ya furaha na utoshelevu unahitaji kuishi upekee wako. Je unaishi kusudi lako na ndoto zako? Au unaishi maisha yoyote yanayokuwa mbele yako. Kwa sababu bado upo hai inakupasa ulitambue na kuanza kuliishi kusudi lako kisha tengeneza na kuitimiza ndoto yako kubwa ambayo umekuwa ukiifikiri kwa muda mrefu.
Uheshimu muda. Muda ndiyo maisha yako. Upo hai kwa sababu ya muda unaendelea kukuweka hapa duniani. Bila muda huu huwezi kufanya chochote na kuwa mtu yule unayetamani kuwa. Bahati mbaya au nzuri ni kuwa muda wako yaani maisha yako ya hapa duniani yana ukomo. Hivyo baada ya kutambua kitu sahihi cha kufanya(kusudi na ndoto) usipoteze muda tena wa kuhangaika na vitu vingine. Tumia muda wako mwingi kuishi kusudi na ndoto zako.
Usikate tamaa. Sumu kubwa ya watu kutokuwa wale waliotakiwa kuwa ni kukata tamaa. Kuishi maisha yenye mafanikio na utoshelevu haijawahi kuwa kazi rahisi. Inawezekana ulikuwa kwenye njia sahihi kabisa ukiishi kusudi lako na ndoto zako lakini kwa sababu ya ugumu uliokutana nao umekufa moyo. Una nafasi ya kufika unakotaka, inuka na endelea na safari. Mafanikio yako yapo karibu sana na pale unapotaka kukata tamaa.
Hakuna kizuizi cha ziada. Kuna kizuizi gani unakiona kikikuzia kutofika kule unakotarajia? Je ni mataji? Je ni elimu? Je ni rangi yako? Je ni historia ya familia yako kuto kuwa na mafanikio? Hakuna kizuizi kingine cha ziada zaidi ya kile unachokiweka mwenyewe kwenye akili yako. Kama hujafanikiwa kufika unakotaka basi tambua ni kwa sababu ya mipaka unayojiwekea ndani yako. Pale unaposema kwa elimu yangu hii siwezi basi ndivyo itakavyokuwa. Kuanzia sasa tambua kuwa hakuna kizuizi chochote cha kukufanya usifike utakako.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kimeelezea kiundani kuhusu unavyoweza kubadilisha maisha yako muda wowote na kufikia kwenye uhalisia wako. Kupitia kitabu hiki utatambua hatua za kufuata kutambua kusudi lako, utatengeneza ndoto yako kubwa na mbinu za kuitimiza na jinsi unavyoweza kutumia muda wako vyema kufanya makubwa. Hiki ni kitabu ambacho hutakiwi kukikosa maishani mwako kama kweli unahitaji kuishi maisha yako halisi. Kitabu hiki kinapatikana kwa sh. 10,000/ tu, piga simu 0752 206 899 kukipata leo.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz