Tumia Macho Haya Kufika Safari Yoyote Ile, Hata Ukiwa Umelala Usingizi.


Categories :

Macho yako ya nyama hutumiaka kutazama na kuona njia au vitu. Ni kwa kupitia macho yako ndipo unapoweza kukanyaga sehemu sahihi ya barabara na kufanikiwa kufika safari yako. Lakini ukishachoka na kuamua kulala, hayawezi kuona tena chochote kwani hufumba na hivyo huwezi kufanya safari yoyote.

Lakini una macho mengine ambayo yenyewe yana uwezo wa kuona mbali zaidi kuliko macho yako mawili. Macho hayo huendelea kufumbua hata kama umelala usingizi na hivyo kuendelea na safari na asubuhi macho yako ya nyama yatakapofumbua macho hayo mengine hukuambia yamesafiri mpaka wapi. Haya ni macho ambayo yenyewe yakififia, hata macho yako ya nyama hayawezi kuona vizuri. Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako lazima macho haya yaone sawasawa. Haya ni macho ya AKILINI.

Akili ina macho ambayo yanaona kwa ukubwa zaidi kuliko macho hayo mawili unayoyafahamu. Ni akili ambayo inaweza kuona vitu hata vile ambavyo bado havijatokea. Inaweza kuona vitu ambavyo vinaweza kutokea mwakani, miaka mitano, kumi ishirini, hamsini au zaidi. Kumbe haya ni macho ambayo yanayokuwezesha kufanya mambo makubwa maishani. Hakuna chochote unachoweza kukifanya na kukuiona masihani mwako kama macho yako ya akili hayajaona.

Tofauti mojawapo kubwa inayotokea kati ya watu waliofanikiwa na walioshindwa ni kwenye macho haya ya akilini. Waliofanikiwa wana akili ambazo zinaona mbali na kwa ukubwa sana ambazo zinawasaidi kujua wapi inabidi waelekee ili waweza kupata matokeo makubwa. Macho ya akili ya walioshindwa hufifia na hivyo kutokuwa wazi kabisa kujua ni nini wanakihitaji maishani mwao. Kwa macho yao ya akilini kufifia, wameishia kufanya vitu vya kawaida na kuwa na maisha ya kawaida.

Kuna maisha ya mafanikio makubwa unayoyatamani kuyapata, kiuchumi, kikazi, kiafaya, mahusiano na binafsi; ili uweze kuyapata hayo, lazima macho ya akili yako yafumbuke na kutazama wazi nini unakitaka, wapi unataka kufika na yaamini kuwa umeshavipata na kufika. Sababu mojawapo iliyokufanya ushindwe kupata vile ulivyovitamani siku nyingi ni kutofumbua macho yako ya akili vizuri. Hivi ndivyo unavyoweza kufumbua macho yako ya akilini na kufanikiwa kuona na kupata chochote ukitakacho maishani mwako;

Uwazi. Hili ni jambo la kwanza kabisa na muhimu kwenye kupata chochote. Umezoea kufumbua macho zaidi pale unapotaka kukiona kitu kwa usahihi zaidi. Ifanye akili yako itambue kwa wazi kabisa nini unakitaka maishani mwako. Kama ni pesa akili yako ione kabisa kiasi unachohitaji kukipata. Hapo ndipo itakapoweza kukupeleka kupata kiasi hicho.

Imani. Unakipata chochote maishani pale ambapo akili yako inakipokea na kukiamini. Baada ya kujua kwa wazi nini unakitaka, jenga imani kuwa una uwezo ndani yako wa kupata chochote.

Yaandike mara kwa mara unayoyataka. Kuna nguvu kubwa inaongezeka akilini mwako na kupata unachokitaka pale unapochukua hatua ya kuandika vile unavyovitaka mara kwa mara. Andika asubuhi, mchana na jioni kile unachokitaka ukipate maishani mwako.

Ndugu jambo mojawapo kubwa unalotakiwa kulifanya ili uweze kupiga hatua kubwa, ni kuhakikisha akili inafumbua na kuona vizuri wapi unakoelekea na kuna nini mwisho wa safari. Amsha uwezo ni mtandao uliokutengenezea mazingira ya kuhakikisha unapata maarifa na miongozo sahihi ya akili yako na  kuwa na uwezo wa kukipata chochote unachotaka maishani. Kwa kujiunga na kundi hili maalumu la wasap utapata makala na dondoo kila siku, semina, miongozo, usimamizi, hamasa, ushauri na vingine vingi vitakavyokufanya macho yako ya akilini yaone na kuyapata makubwa.

Gharama za kujiunga na kundi hili ni shilingi elfu kumi(sh 10,000) ambayo unaweza pia kulipia kwa awamu mbili. Hii sio fursa ya kujiuliza mara mbili, jiunge sasa na kuanza kufaidi makubwa yaliyopo. Kujiunga na mtandao bonyeza kiunganishi hapo chini.

https://chat.whatsapp.com/Dx1HF02stFq2LxIqoRTAUD

Kwa mawasiliano zaidi usisite kuwasiliana name kupitia simu 0752206899/0714301952.

Asante.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *