Usihangaike Kunyoosha Kivuli Cha Mti; Nyoosha Mti Wenyewe.
Itakuwa ni ajabu sana kwako kama utamuona mtu yupo ‘busy’ akijaribu kunyoosha kivuli cha mlingoti kwa sababu taswira yake inaonyesha imepinda akitarjia atafanikiwa kufanya hivyo na kuunyoosha mlingoti huo. Mtu huyo ungefikiri kuwa atakuwa na upungufu wa akili.
Lakini jambo hili lipo katika jamii na ndilo linalochangia kushindwa kwa watu wengi. Wengi wanahangaika na kunyoosha vivuli vya milingoti wakitarajia milingoti hiyo kunyooka. Kunyoosha vivuli maishani ni kuhangaika kurekebisha matokeo badala ya vyanzo vya matokeo. Huku ni kupoteza muda na nguvu ambavyo wengi wamefanya. Usitarajie matokeo ya tofauti katika maisha yako kama hutabadilisha visababishi vya matokeo hayo.
Inawezekana umekuwa ukijaribu kunyoosha vivuli maishani mwako kwa muda mrefu kwa kujua au kuto kuja. Pia naamini unahitaji kupata mabadiliko kwenye matokeo ambayo hujayafurahia kwa muda mrefu, basi nakuambia siri ya kubadilisha matokeo hayo ni kunyoosha mlingoti na sio kivuli chake. Hivi ndivyo unavyoweza kunyoosha milongoti ya maisha yako na sio vivuli vyake;
Usiyachukie matokeo unayoyapata, tazama hatua unazochukua. Hakuna matokeo unayoweza kupata bila kuchukua hatua. Hata kutokufanya jambo ni kuchukua hatua ya kutokufanya. Hivyo chochote kinachotokea maishani mwako, ni kwa sababu ya hutua fulani ulizowahi kuchukua. Je huwa unaahirisha sana mambo kiasi cha kutipata matokeo ya kutosha; yaani baada ya kufanya jambo hilo mara nne kwa juma, wewe unaahirisha mara mbili na hivyo kupata matokeo ya siku mbili tu? Katika hali kama hii usihangaike eti kwa nini unapata matokeo kiduchu, badala yake boresha hatua unazochukua.
Usilalamike kwa nini unabaki masikini, jiulize ni thamani gani unaitoa kwa wengine? Utajiri ni zao la thamni unayotoa kwa watu wengine. Kam bado masikini, jitihada pekee zitakazokutoa huko ni kuanzisha thamani au kuongeza mpaka watu wawe tayari kukulipa kwa utele. Hivyo kulalamikia umasikini ungali hutoi thamani ya kutosha, ni kuweka jitihada za kunyoosha kivuli badala ya mlingoti.
Usilalamike biashara yako haina wateja, je ni kwa namna gani unawajali wateja wako? Moja kati ya vitu vinavyofanya biashara yako iendelee kuwepo ni wateja amabo watanunua. Bila wateja hakuna mauzo, kama hakuna mauzo hakuna mzunguko wa pesa na hivyo biashara kufa. Hivyo biashara yako lazima ihangaike kuhakikisha inampa thamani ya kutosha mteja wako na ili anunue leo na kesho na kuwa mteja wa kudumua. Biashara yako kuhangaika na vitu vingine kama kutumia faida badala kumfanya mteja wako mfalme, ni kuhangaika kunyoosha kivuli badala ya mlingoti.
Usilalamike kwa nini watu hawakupendi, jiulize ni kwa kiasi gani unawajali watu wengine? Kile unachokitoa kwa watu wengine ndicho kinachokurudia. Ukipna watu wengi wanakuchukuia, jiulize wewe unawapa nini? Upendo au chuki? Hivyo kuendelea kulalamika kuwa watu sio wazuri ungali ubaya unaanzia kwako, ni kujaribu kuonyoosha kiculi badala ya nguzo.
Usilalamike mbona kila nikianzisha jambo sifanikiwi, balu jiulize unavumilia kwa kiasi gani? Waswahili husema mambo mazuri hayahitaji haraka. Kumbe ukitaka upate mafanikio huna budi kuwa mvumilivu, hata pale mambo yatakapokuwa magumu, jipo moyo na kuendelea kuweka nguvu, kama upo njia sahihi hakika utapata matokeo. Kujaribu na kuacha kisha kulalamika kwa nini hufanikiwi, huku ni kunyoosha kivuli badala ya mlingoti.
Ndugu! Tafakari ni maeneo gani ya maisha yako umekuwa ukinyoosha kivuli badala ya mlingoti. Je ni kwenye biashara na ajira yako? Je kwenye mahusiano? Au hali yako ya kiuchumia? Anza sasa kunyoosha mlingoti katika maeneo hayo badala ya kivuli.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz