Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutambua Uwezo Wako Ulionao na Kupata Utajiri.
“Ni mpaka nazi ivunjwe ndipo uone kitu chenye thamani ndani yake. Kadhalika ni mpaka yai lipasuliwe ndipo unaweza kupata kimiminika chenye thamani ndani yake”
Thamani ya vitu ipo ndani, mara nyingine ni vigumu kuiona thamani hiyo mpaka upate nafasi ya kuchungulia ndani. Kama huifahamu nazi, huwezi ukaijua kwa haraka haraka kama ndani yake kuna unga wenye thamani kubwa. Kadhalika huwezi kujua thamani ya kimiminika cha yai mpaka uvunje ganda lake, ndipo ukutane na chakula kitamu che virutubisho vingi sana.
Hii ndiyo siri ambayo imejificha kwenye vitu vingi. Thamani ya vitu vingi haionekani kirahisi, haionekani kirahisi ukijikita kwa nje. Kwa sababu watu wengi hupenda kuangalia kwa juu juu tu bila kuchunguza vizuri na kujikita kwa ndani. Kwa kufanya hivyo wengi wameshindwa kujua thamani ya vitu vya kukuwezesha kupata thamani kukuwezesha kupiga hatua.
Ndivyo ilivyo kwako, una thamani kubwa sana ndani yako ya uwezo. Thamani hiyo umeendelea kuishi nayo bila ya kuitumia na hivyo kuendelea kuishi maisha ya kawaida. Maisha ya kawaida ni yale yenye mafanikio madogo ambayo hukusitahilo na hayakuridhishi.
Kama ilivyo kwenye nazi na yai kwa thamani zake kuonekana baada ya kubomoa kuta zake ndivyo kwako lazima kuwe na mazingira ambayo yatabomoa ukinzani unaoendelea kuficha uwezo wako ndani yako. Unaweza kujiuliza nia nyundo gani inayoweza kubomoa ukuta uliozunguka uwezo wako? Nyundo hiyo ni changamoto.
Uwezo wenye thamani ya upo ndani yako. Thamani hiyo haiwezi kuonekana mpaka pale mazoea yatakapovunjwa na kudhihirisha nguvu hiyo. Mazoea yamekufanya kuendelea kufanya yale yale kwa kiasi kile kile kila siku. Ni mazoea yaliyokupa matokeo ya kawaida.
Ni changamoto ndizo zinazoweza kukutoa kwenye mazoea na kuvunja kuta zinazozuia uwezo wako kutoka ndani yako na kutoa thamani itakayokuwezesha kupata utajiri. Kumbuka kuwa utajiri unatokana na kutoa thamani. Kama kimazoea umekuwa ukifanya biashara ndogo na kuona kuwa huna uwezo wa kufanya biashara kubwa, huna budi kujipa changamoto sasa ya kuweka lengo kubwa la kutoa thamani kubwa zaidi ambazo zitakufanya ivunje kuta hizo na kuzalisha thamani zaidi katika biashara yako na kupata kipato kikubwa zaidi.
Weka lengo kubwa zaidi. Ili kuondoka na mazoea na kuvunja kuta zinzozunguka uwezo wako na kuzuia uwezo wako, huna budi kuanza kufanya kitu cha utofauti. Moja ya jambo hilo ni lengo kubwa. Kuna mambo ambayo umekuwa ukifanya na kufanikiwa, hayo sasa hayawezi kuvunja kuta na kuamsha uwezo wako zaidi. Huu ni wakati wa kupata changamoto mpya kwa kuweka malengo mapya na makubwa ya kuvunja kuza uwezo wako kisha kuruhusu mafanikio makubwa zaidi.
Badili kauli. Hakuna kinachoweza kubadilika bila bila fikra zako kubadilika. Ona katika fikra yako kuwa kuna kitu kikubwa ndani yako unachoweza kufanya zaidi ya sasa. Ile imani utakayoweka itavunja kuta zote na kufanikiwa makubwa zaidi ya haya.
Vunja mazoea uliyonayo kwa kuweka malengo makubwa za zaidi ya yale uliyozoea ili. Malengo haya yatakusukuma kufikiri na kuweka nguvu zaidi na hivyo kuthibitisha uwezo mkubwa zaidi ambao ulikuwa huutoi.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kinanaeleza kiundani jinsi ulivyoukumbatianuwezo wako bila ya kuuamsha kukupa utajiri ambao ni haki yako. Kitabu hiki pia kimeelezea ni kwa namna gani unaweza kuvunja kuta hizo na kisha kuwa na uwezo wa kutoa thamani kubwa zaidi ya sasa na kukuwezesha kufikia utajiri.
Kitabu hiki ni sh. 10,000/ . Thamani ya mambo yaliyomo hayaendani na bei hiyo lakini kwa kuwa najali mafanikio yako, nimeweka bei hiyo ili ukipate.
Kwa wale wanaopenda nakala tete, unaweza kukipata kitabu hiki kwa kupakua kupitia kiunganishi hapo chini, ukikwama tuwasiliane.
https://www.getvalue.co/prod/amsha_uwezo_wako_halisi
Kwa mawasiliano zaidi piga simu no. 0752206899.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz