Hii Ndiyo Njia Pekee Ya Kuwa Tayari Kupita Kwenye Moto.


Categories :


Mama ambaye mwanae yupo chumbani kwenye nyumba inayoungua moto ana ujasiri wa kujaribu kuingia kwenye chumba hicho ili amuokoe mwanae.

Mtu anayeumwa huwa radhi kuvumilia maumivu makali ya sindano ili apate kupona. Au hata ikitakiwa kukata mwili au kiungo ili aweze kupona, hatua hiyo hufanyika ili kuokoa maisha yake. Ujasiri wa mama kuingia kwenye nyumba inayowaka moto au mgonjwa kuvumilia maumivu ya matibabu hutokana na kuwa na sababu kubwa inayowashawishi kufanya hivyo licha ya hatari au maumivu wanayoyapata.

Kwenye maisha yako kuna uwezekano wa kupata chochote unachotaka. Hata vile ambavyo umeona ni vya watu fulani, na wewe unaweza kuvipata pia. Lakini vitu vizuri pia vina gharama kubwa ya kulipa. Licha ya kuwa na uwezekano wa kuvipata lakini siyo rahisi, kuna gharama za kulipa. Kwa sababu ya gahrama hizo kuwa kubwa pia, watu wengi wameishia kuyatamani mafanikio bila kufanikiwa kulipa gharama.


Kulipa gharama kwa ajili ya kupata mafanikio makubwa ambayo mtu angetamani kuyapata ni sawa na kuwa tayari kupita kwenye moto. Hii ni kwa sababu ya safari hii kuwa ngumu yenye changamoto nyingi. Ili kuweza kufika kileleni mwa safari hii huna budi kujitoa hasa kupitia magumu yote, huku ni kuwa tayari kupita kwenye moto. Kuna njia moja ya uhakika ya kukuwezesha kupita kwenye moto, njia hiyo ni kuwa na kwa nini kubwa.

KWA NINI kubwa ni sababu kubwa inayokulazimisha wewe ukibali kujitoa kwenye safari hiyo ngumu. Hii ni sababu itakayokufanya uamke mapema na kuacha usingizi mzito na mtamu wa asubuhi. Hii ni sababu itakayozidi uzito wa utamu wa starehe kama kufuata vileo au kufuatilia michezo. Hii ni sababu itakayokufanya uweke akiba hata kama unaitamani hiyo fedha kufanyia viti vingine. Sababu hiyo ni ipi?

Kila mtu anaweza kuwa na kwa nini yake. Je ya kwako ni umasikini uliokuzunguka kiasi cha kuuchukia na kutaka kuubadilisha utajiri? Je ya kwako ni tatizo fulani linalowakabili kama elimu, na hivyo kujitoa kuhakikisha unawatoa watu kwenye dimbwi la ujinga? Je ya kwako ni kuona watu wanakuwa huru kutoka kweny ugonjwa fulani unaowatesa watu wengi.

Kwa nini yako inaweza kuwa maumivu fulani unayotaka kuyakomesha au hamu ya kitu unachotaka kukipata. Utaipata kwa nini yako sahihi kutoka ndani yako. Kuna kitu ukikiona kinakuushi sana na unona una wajibu na uwezo wa kukirekebisha. Au kuna kitu ambacho unaona hutaridhika kama utaondoka hapa dunia bila kukipata au kukifanya. Moyo wako una siri hiyo. Kwa nini yako huungana na kusudi lako ambayo ni sababu ya wewe kuwepo hapa duniani.

Kuishi kusudi lako kikamilifu ndiyo njia pekee ya kupata mafanikio makubwa hapa duniani. Kumbe kitu cha kwanza kabisha ili kuweza kufikia mafanikio makubwa hapa duniani ni kutambua kwa nini upo hapa duniani na nini unacho cha kukuwezesha kutimiza kwa nini hiyo.

Chukua hatua: Kaa chini na tafakari kwa kina, kitu ambacho una shauku kubwa ya kukifanya au kukipata katika maisha yako. Weka mipango sasa ya kukifanya na kukipata kitu hicho huku ukiwa tayari kupita kwenye moto wowote mradi tu ukipate. Huko ndiyo kujitoa. Una uwezo wa kukipata chochote, tafuta KWA NINI yako kubwa.

Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kimeelezea kiundani kuhusu kutambua kusudi lako(kwa nini) na kuliishi. Jipatie nakala yako leo ili uweze kupata chochote unachotaka. Kupata kitabu hiki piga simu 0752 206 899.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *