Unaweza Kukipata Hiki Ulichokitamani Kwa Siku Nyingi.
Kuna kitu ambacho ni tamanio la karibu kila mtu hapa duniani. Kitu hicho kimekuwa kikichukua muda mwingi wa maisha ya mtu kutafutwa. Na mambo mengi ya mtu huyo hukaa vizuri akishakipata kitu hicho. Akishakipata na yeye huona wa thamani hapa duniani. Naamini unatamani ujue kitu hicho, nami nakuambia kuwa kitu hicho ni utajiri.
Neno utajiri limekuwa likipendwa kusikiwa masikioni mwa watu wengi. Pia utajiri kimekuwa ni kitu kinachotafutwa kwa nguvu kubwa karibu na kila mtu katika maisha yake. Utajiri unaoongelewa hapa ni ule uhuru wa kifedha/mali ambao mtu huwa nao. Mtu anapofikia utajiri, fedha zinakuwa sio kikwazo tena kufanya mambo yake. Kuwa tajiri ni kuwa huru kununua chochote, kwa na uwezo wa kwenda popote, chochote nk.
Licha ya utajiri kutokuwa vitu vyote lakini ni vitu vingi. Matatizo mengi yanayokukumba yanaweza kutatulika kwa kuwa na fedha. Kwa mfano afya, maarifa, mahusiano, chakula, starehe nk.
Kwa sababu utajiri umekuwa tamanio la watu wengi, jitihada nyingi ambazo binadamu amekuwa akizifanya zimelenga kujipatia utajiri. Kulithibitisha hilo, kumekuwa na matukio mbalimbali yanayotokea yakiashiria watu wakitafuta utajiri hata kama njia zisizo sahihi.
Kumekuwa na imani za kishirikina zikifanywa kwa ajili ya kujipatia utajiri. Kukumbuka mauaji ya albino yakihusishwa kusaidia kupata utajiri, na watu walikuwa tayari kukamilisha unyama huo ili waweze kupata utajiri. Hivi karibuni Nchini …..limeibuka suala la kuuza vidole vya miguu kwa bei kubwa, kwa sababu ya kiu hiyo, watu wamekuwa radhi kubaki bila vidole ili waupate utajiri. Pia kwa sasa wapo busy na michezo ya bahati nasibu kwa kutamani zile fedha nyingi zinazotangazwa.
Licha ya kuwa na jitihada mbalimbali za kupata utajiri zilizo halali na zisizo halali lakini bado asilimia kubwa ya watu hawafikii utajiri yaani uhuru wa kifedha. Njia halali kama ajira hazijaweza kuwapa utajiri watu. Ndiyo maana matajiri wengi hawajaupata utajiri huo kwa njia ya ajira. Kuna njia moja ambayo jitihada zake zinaweza zikimhakikishia mtu utajiri. Njia hiyo ni kupitia biashara yenye mafanikio.
Biashara yenye mafanikio.
Biashara ni njia maarufu iliyowafikisha watu wengi kwenye utajiri. Biashara ni kitendo cha kuuza thamani kwa watu wengine ili kupata faida. Thamani hiyo inaweza kuwa bidhaa au huduma. Njia hii imewawezesha watu wengi kufikia utajiri wao kwa sababu ya kuwa nafasi ya kukua kadri unavyoendelea kutoa thamani. Hivyo kadri mtu anavyozidi kuongeza thamani ndivyo anavyozidi kuongeza kipato.
Imekuwa rahisi kwa mtu kupata utajiri kupitia biashara kwa sababu ya uwezo wa kukuza thamani anayoitoa hata bila ya uwepo wake. Unaweza kuendesha biashara zaidi ya moja tena maeneo tofauti kwa mafanikio makubwa hata bila ya yeye kuwepo hapo tofauti na ajira ilivyo.
licha ya njia hii kuwa na uhakika wa kuwafikisha watu kwenye utajiri, lakini watu wengi wameshindwa kuanzisha biashara na hata wale walioanzisha biashara, zinakufa ndani ya muda mfupi huku nyingi zikiwa ICU. Hiki ndicho kimekuwa kikwazo cha watu wengi kufikia uhuru wao wa kifedha.
Biashara gani nianzishe? Nitapata wapi mtaji wa biashara? Namna gani niiendeshe na kuikuza biashara kufikia mafanikio makubwa? Haya ni baadhi ya maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza bila ya kuwa na majibu sahihi. Kwa kuwa nakujali na kukutaka upate mafanikio ya utajiri katika maisha yako, Amsha Uwezo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia tar 11 – 20 Julai 2022 kwa njia ya mtandao wa wasap itakayokupa majibu ya maswali hayo yote. Semina hii imebeba kicha UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
Kupitia semina hiyo utapata wazo la biashara ambalo litakuwezesha kupata wazo la kuianzisha na kuikuza biashara yako na kisha kupata mafanikio makubwa. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi(sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Wakati wa kupata ulichokitamani siku nyingi umefika.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz