Wewe Pia Una Sehemu Katika Utele Huu.
Licha ya simba kuendelea kuwawinda na kuwala swala kila siku swala hao hawajawahi kuisha. Licha ya watu kuvua na kula samaki kila siku lakini bahari haijawahi kuishiwa samaki. Licha ya wanyama kuendelea kuvuta hewa ya oksjeni kila siku lakini hewa hiyo haijawahi kuisha. Hivi ni baadhi ya viashiria vya kuwa dunia ina utele.
Umekuwa ukiamini maishani mwako kuwa dunia ina uhaba. Kwanza kwa kuona kuna watu fulani ndiyo wanaweza kufanya mambo makubwa na wewe huna uwezo wa kufanya, umejenga imani kuwa wewe una uhaba wa uwezo. Ulipowaona matajiri wakiwa na fedha na mali nyingi nakuona wewe huwezi kuwa tajiri kwa kuwa utajiri wote umechukuliwa na wachache, hii imekuwa ni imani ya uhaba.
Kama ulivyoona kwenye utangulizi hapo juu kuwa dunia huwa haiishiwi bali ina utele kila wakati. Hivyo na wewe unaweza kupata na kufanya chochote unachotaka hapa duniani.
Moja ya utele ambao watu wameupata ni utajiri kama mali na fedha. Njia kuu waliyoitumia kupata utajiri huu ni biashara kwa sababu ya uwezo wa kukua haraka inapoendeshwa vizuri.
Licha ya watu kuwa na njia hii ya wazi ya kufikia utajiri, lakini wengi wameshindwa kuitumia. Moja ya sababu ya kutopata utajiri huo ni wao kufikiri kuwa biashara zote zimeshachukuliwa na hakuna biashara unayoweza kuifanya wanayoweza kuifanya.
Je wewe ni miongoni mwa watu wenye mtaji wa kuanzishia biashara lakini umekosa wazo la biashara gani waifanye? Je wewe ni miongoni mwa watu walioamua kuiga kufanya biashara yoyote ile baada ya kuamini inawafaa lakini wakaishia kushindwa vibaya?
Napenda kukutoa hofu kuwa dunia ina utele, kila mtu anaweza kupata wazo la biashara akaanzisha na kuikuza kwa mafanikio makubwa. Hakuna biashara moja inayomfaa kila mtu, hivyo kwa sababu dunia ina utele wewe pia utapata biashara inayokufaa wewe.
Hatua ya kwanza ya kupata wazo bora la biashara ni kujua kitu unachopenda kukifanya au kukifuatilia. Je kuna kitu ukikisikia utaacha chochote ulichokuwa unakiafanya ili ukifuatilie au ukifanye hicho? Je kuna kitu unachopenda kukifanya kiasi cha kuwa tayari kukifanya hata bila malipo? Je kuna kuna kitu unapenda kukifanya na ukiifanya unafanya kwa viwango vya juu sana? Hakika utakuwa na jibu chanya kuhusu hayo maswali. Hii ni hatua ya kwanza na muhimu katika kupata wazo la biashara yanye mafanikio.
Kuna umuhimu mkubwa wa wazo biashara yako kutoka kwenye kitu unachokipenda. Safari ya biashara yenye mafanikio makubwa haijawahi kuwa rahisi hata siku moja, hivyo wale wanaostahimili na kufanikiwa ni wale ambao biashara zao zimetokana na vitu wanavyovipenda.
Hii ni hatua ya kwanza ya kupata wazo bora la biashara yenye mafanikio. Kuna hatua nyingine tatu za kukamilisha zoezi hilo muhimu pale unapotaka kuanzisha biashara. Ndugu! Ili uweze kujifunza hatua hizi nne na kuanzisha biashara yako, AmshaUwezo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022.
Maada ya semina hii ni UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
Kupitia semina hiyo utapata wazo la biashara ambalo litakuwezesha kuianzisha na kuikuza biashara yako na kisha kupata mafanikio makubwa. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumula wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi(sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Wakati wa kufaidi utele wa dunia umefika. Usipange kukosa fursa hii.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz