Hata Wewe Una Uwezo Huo.
Mimi sio mtu wa kufanya biashara! Biashara zina wenyewe bwana. Biashara za kabila fulani, biashara za uko fulani. Biashara zina wenyewe bwana.
Haya ni maneno ambayo huwa yanasikiwa yakisemwa na watu. Watu hawa wanaamini kuwa kuna watu fulani ambao ndiyo wanaostahili kufanya biashara. Yaani hata kama kuna watu wengine tofauti na wale unaowaona wanastahili basi ni wa biashara ndogo ndogo.
Hii ni dhana ambayo imewanyima watu wengi sana kuanzisha na kukuza biashara zenye mafanikio makubwa katika maisha yao. Mtazamo huu umeleta usingizi mzito kwenye uwezo walionao watu. Unaposema wewe hustahili au huna uwezo wa kuanzisha au kukuza biashara ndivyo unavyozidi kuubembeleza uwezo wako mkubwa wa kufanya chochote uliopo ndani yako.
Mtazamo una mchango mkubwa sana kwenye kutumia uwezo wako uliopo ndani yako. Mtazamo sahihi unahitajika ili kuamsha nguvu za kuanzisha na kukuza biashara. Amini unaweza kufanikiwa katika biashara. Kama unawaona watu wamefanikiwa kwenye biashara, na wewe unaweza kufanikiwa katika eneo lako la biashara.
Biashara ni uwezo wa kutoa thamani kwa watu wengine na wao wakawa tayari kulipia thamani hiyo. Thamani hiyo inaweza kuwa bidhaa au huduma. Kila mtu yupo hapa duniani kutoa thamani kwa watu wengine na yeye kupokea thamani kutoka kwa watu wengine. Hivyo kuna biashara yenye mafanikio ambayo dunia inasubiri uianzishe na kukikuza.
Pamoja na mtazamo ambao unatawaliwa na akili, kuna maeneo mengine manne ambayo yanaathiri matumizi ya uwezo ambao upo ndani yako katika kufanikiwa kibiashara. Maeneo mengine ni mwili, hisia, roho na tabia.
Neno uwezo limekuwa likitafsiriwa kwa ubaya na watu wengi. Wengi wamefikiri uwezo huu unaozungumziwa ni wa akili tu yaani ubongo au mwili tu. Lakini hii si tafsiri kamili ya uwezo kwani unahitaji kuhusisha viungo vyote vitano. Nguvu za mwili pekee hazitakusaidia kufanya biashara yenye mafanikio.
Kwa kutegemea eneo moja au mawili tu ya wengi wamepata changamoto kubwa katika kuendesha biashara zao. Kumbe wewe ili uweze kuwa na biashara yenye mafanikio unahitaji kuamsha maeneo hayo yote. Unaamshaje maeneo hayo mengine?
Ili uweze kuamsha uwezo wako kamili na kufanikiwa katika biashara, inatakiwa viungo vyote vitano viamshwe. Je unawezaje kuamsha uwezo wako uliolala ndani yako? AmshaUwezo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022.
Maada ya semina hii ni UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza viungo vya uwezo kiundani na kisha kupata wazo la biashara ambalo litakuwezesha kuianzisha na kuikuza biashara yako na kisha kupata mafanikio makubwa. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi(sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Wakati wa kufaidi utele wa dunia umefika. Usipange kukosa fursa hii. Amsha uwezo wako na anzisha biashara yenye mafanikio.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz