Haya Ndiyo Macho Yanayoona Biashara Yenye Mafanikio.
Bundi anauwezo wa kuona mbali mara kumi zaidi ya anavyoweza kuona binadamu. Hii inampa uwezo wa yeye kuona mawindo hata kwa umbali mrefu zaidi.
Lakini licha ya bundi kumzidi binadamu umbali anaouona kwa kwa macho, binadamu amemzidi bundi umbali wa kuona kwa namna nyingine. Binadamu ana uwezo wa kuona kwa namna hiyo mara dufu ya bundi anavyoweza kuona. Namna hiyo ni kwa kutumia akili.
Licha ya bundi kuwa na uwezo wa kuona mbali mara kumi zaidi ya binadamu lakini akili ya bindamu inaweza kuona hata miaka kumi au zaidi ya bundi. Haya ndiyo macho unayotakiwa kutumia kuiona biashara yako ili uweze kufanikiwa. Haya yanaitwa maono ya biashara.
Biashara zenye maona zinajiona zipo wapi baada ya mwaka mmoja, miaka mitano, miaka kumi hata hamsini ijayo. Unaiona biashara yako ikikua kwa kiasi gani baada ya muda fulani? Unaiona biashara yako ikitatua tatizo gani kubwa linalosumbua jamii? Unaona picha gani kwenye biashara uliyoianzisha?
Maono ya biashara ni msingi muhimu sana katika kujenga biashara yenye mafanikio. Ili uweze kuianzisha na kuikuza biashara yako, lazima uhakikishe unajua hatima ya biashara yako. Huu utakuwa mwongozo wa biashara yako. Biashara yenye maono huwa hamasa na jitihada kubwa za kuhakikisha inakua.
Watu wengi wamekuwa wakianzisha biashara ambazo hawajui zinakoelekea. Wanaanzisha kwa sababu wanaoana wengine wameanzisha. Au kwa sababu wamesikia zitawapa faida. Hakuna biashara itakayodumua na kutoa matunda kama haijajengwa kwenye misingi imara ikiwemo maono.
Malengo yoyote ya biashara yako lazima yatokane na maono ya biashara hiyo. Huwezi kukisia utembee kwa kasi gani kama hujui wapi unafika. Baada ya kuwa na picha ya wapi inabidi ufike kwenye biashara yako, ndipo unapoweza kuweka malengo yatakayokuwezesha kuifikia picha hiyo.
Si maono pekee bali kuna msingi mwingine ambao biashara yako ikifanikiwa kujengwa kwenye misingi hiyo miwili itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa.
Ndugu! Mtandao wa AmshaUwezo upo tayari kuhakikisha biashara yako inajengwa kwenye misingi hiyo miwili muhimu. Hivyo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada “UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO”
Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kiundani misingi miwili muhimu ya biashara na kuhakikisha unaijenga biashara utakayoianzisha au uliyonayo kwenye misingi hiyo.
Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Biashara isiyo na maono inajiandaa kufa. Usipange kukosa fursa hii.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz