Biashara Yako Itafanikiwa Kama Utaitengenezea Kitu Hiki.


Categories :



Ni tamaa ya kila mwanadamu kufanikiwa kwenye kila jambo. Hata kukata tamaa huja baadaye sana baada ya kushindwa kuweka juhudi kwenye jitihada za mafanikio aliyokuwa anayatamani. Moja ya tamaa ya mafanikio ambayo watu wanayo ni kufanikiwa katika biashara zao.

Biashara imeonekana kuwa ndiyo sululisho kubwa la mtu kupata kipato chenye uhakika na mwisho kufikia uhuru wa kifedha. Lakini licha ya biashara kuwa sluu, hata hivyo biashara nyingi zimegeuka kuwa miiba kwa watu wengi.

Wapo walioanzisha biashara lakini zimekufa baada ya mud mfupi tu. Wapo ambao wamekuwa wakibadilisha biashara kila wakati; baada ya moja kutofanya vizuri, wanafunga na kuanzisha nyingine. Kwa namna hii wamepoteza nguvu, fedha, muda na utulivu. Pia kuna biashara nyingi ambazo kwa sasa zipo hoi sana. Moja ya changamoto inayosababisha biashara nyingi kufa ni kukosa mfumo.

Business teamwork with mechanism system. Vector Illustration



Itazame dunia! Vitu vingi vinafanikiwa kuendeshwa kwa mafanikio makubwa kwa sababu ya mifumo ambayo tayari ipo. Tunapata usiku na mchana kwa sababu ya kuwa na mfumo dunia kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake. Utazame mwili; unafanikiwa kuwa hai na kufurahia maisha kwa sababu mwili kuendeshwa kwa mifumo mbalimbali kama mfumo wa upumuaji, mmeng’enyo wa chakula, kusukuma damu, utoaji taka mwili, uzalishaji nk. Na mfumo mmoja ukilorofisha mwili wako huwa kwenye shida.

Ndivyo inavyotakiwa kwenye biashara yako ili iwe yenye mafanikio makubwa. Biashara nayo ni kama kiumbe hai, inahitaji mfumo ili iishi na kukua. Kuna maeneo matatu muhimu ya kujengenea mfumo biashara yako.

Eneo la kwanza ni Uendeshaji na Uzalishaji. Hili ni eneo muhimu sana la kuweka utaratibu bora wa namana biashara yako inavyoendeshwa. Wafanyabiashara wengi hawana utaratibu maalumu (mfumo) wa kuendesha shughuli za biashara au uzalishaji mali. Hii ndiyo imekuwa ni sababu mojawapo ya biashara kufanya vizuri akiwepo mtu fulani, hasa mmiliki. Mmiliki usipokuwepo, anayechukua majukua anaendesha kama anavyojua yeye na mwisho wa siku mauzo yanapungua na wateja kukimbia biashara pia.

Je vipi ubora wa bidhaa unazozalisha au nunua? Je zina ubora uleule kila siku? Chukualia mfano wa mtu anayetengeneza chapati mgahawani, je kwa nini ubora wa chapati hizo unatofautiana kila siku? Majibu ya maswali haya yote ni kutokuwa na mfumo wa Uendeshaji na Uzalishaji. Kama kweli unataka uanzishe aua uiendeleze biashara yenye mafanikio huna budi kuiwekea mfumo mzuri wa Uendeshaji na Uzalishaji.

Ndugu! Mtandao wa AmshaUwezo inakujali wewe na biashara yako. Upo tayari kuhakikisha unakufundisha kwa kina kuhusu mfumo wa biashara yoyote ile unayoifanya ili ifikie matamanio uliyonayo.

Hivyo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada “UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO”

Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kwa kina kabisa maeneo matatu muhimu ya biashara yako ya kutengenezea mfumo.

Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kisha kulitumia.

Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7

Biashara isiyo na Kliniki inajiandaa kufa. Usikise fursa hii muhimu ya kujua namba za biashara.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *