Hivi Ndivyo Chuma Ulete Wa Biashara Yako Alivyozaliwa.


Categories :


Moja ya malalamiko mengi ambayo wafanyabiashara waliyonayo ni kupotea kwa fedha za kwa njia ya imani za kishirikina(chuma ulete). Wafanyabiashara wa karibu au watu fulani wanaoizunguka biashara za watu hao ndiyo wamekuwa wakishutumiwa kuhusika kuchukua fedha za biashara za watu kwa njia ya ushirikina.

Wafanyabiashara kadhaa wamedai kushindwa kukuza biashara zao na baadaye kufa kabisa kwa sababu ya uhuma ulete. Inawezekana hata wewe unayesoma hapa ni miongoni mwa watu waliokutana na uhuma ulete au umewasikia wakisema. Je uhuma ulete kweli yopo?

Je umewahi kujiuliza swali hili? Kama uhuma ulete yupo kwa nini anahangaika na fedha ndogo za biashara yako badala ya kwenda kuchota fedha nyingi zilizopo benki?
Kwa sababu ni kweli fedha huwa zinapotea kwenye biashara yako, hii inathibitisha kuwa uhuma ulete yupo, lakini ametengenezwa wewe mwenyewe.

Kwenye taasisi za kifedha kama benki, fedha hazipotei kwa sababu kuna mfumo unaosimamia fedha. Mfumo huo huweka bayana fedha yoyote inayoingia na inayotoka bila kujali udogo au ukubwa wake. Ikitokea hesabu tarajiwa haifanani na iliyopo kwenye, ni lazima itafutwe kwa namna yoyote ile mpaka ipatikane. Jambo hili hufanyika hata kwa fedha ndo kam senti hamsini.

Je biashara yako ina utaratibu gani wa kuthibiti mzunguko wa fedha; yaani fedha inayoingia na kutoka? Je wewe pia ni biashara kiasi kwamba unaweza kuchukua kiasi fulani cha fedha na kusema utarudisha lakini hufanyi hivyo? Je utajuaje kama mfanyakazi wako amechukua fedha bila kuirudisha? Mazingira hayo uliyoyatengeneza ya kutokuwa na uthibiti wowote wa fedha kwenye biashara yako ndiyo uhuma ulete mwenyewe.

Ndugu! Hujawahi kuwa na biashara inayoenda vizuri mwanzoni huku ukiona na faida kabisa, lakini baada ya muda ukaendelea kuuza lakini huoni fedha? Kama unauza huna budi kuziona fedha lakini kama huzioni inamaanisha kuwa kuna sehemu biashara yako inavujisha fedha.

Sluu ya uhuma ulete ni kuanzisha mfumo ambao utatambua na kuthibiti kila fedha inayoingia na kutoka kwenye biashara yako. Mfumo huo utakusaidia kufanya tathmini ya biashara yako kutambua mwenendo wake.

Nitatengenezaje mfumo huu? Hili linaweza kuwa ni swali unalojiuliza sasa! Usihofu; mtandao wa AmshUwezo upo tayari kukuwezesha katika hilo kwa kuhakikisha unapata wazo bora la biashara yako kisha kuitengenezea mfumo utakaohakikisha uhuma ulete hazaliwi. Si hivyo tu bali na wewe uliyopo kwenye biashara mtandao huo utakuwezesha kumuondoa bukula huyo na kuifanya biashara yako ikue na kuifikia mafanikio makubwa.

Hivyo imekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada “UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO”

Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kwa kina kabisa kuhusu uthibiti wa fedha kwenye biashara yako kisha kuiona faida ya biashara yako hata kama inafanywa na mtu mwingine.

Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kisha kulitumia.

Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7

Biashara iliyo na chuma ulete inajiandaa kufa. Usikose fursa hii muhimu ya muondoa chuma ulete kwenye  biashara yako.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *