Hii Ndiyo Siri Ya Kupata Matokeo.
Kuni zinapokubali kuungua kisha kubadilika kuwa majivu, ndipo unapoweza kupata joto lililofichwa ndani ya kuni hizo. Kadhalika mbegu ya mti inapokubali kufa na kubadilika kuwa mche, ndipo tunapoweza kupata mti mkubwa uliofichwa ndani ya mbegu hiyo.
Ukiuangalia ukuni kabla haujashika moto huwezi kudhania utazalisha joto la kutosha kuivisha chakula. Vivo hivyo ukiiangalia mbegu ya mti kabla haijakubali kuwa mche unaweza kuidharau kama inaweza kuwa mti na hata msitu baadaye.
Katika mifano miwili hapo juu, kuna kitu kimoja muhimu kinachotokea ili kuweza kupata matokeo mazuri yenye faida. Hiki pia ndicho kitu muhimu sana kinachohitajika ili kupata matokeo katika maisha hako. Hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio unayoyatafuta kila siku. Kitu hicho ni MABADILIKO.
Ukuni ulihitajika kubadilika kwenda kwenye majivu ili utoe joto, mbegu ilihitajika ibadilike kuwa mche ndipo upate mti. Kama kuna kitu umekuwa ukikitamani kukipata siku nyingi na hujakipata, basi sababu mojawapo ni kuwa hujafanya mabadiliko kabisa au mabadiliko hayo hayajakamilika.
Kanuni ya kwanza ya mwendo ya Newton inasema ‘’Kila kitu kiataendelea kubaki kwenye hali yake ya awali mpaka pale nguvu kutoka nje itakapowekwa’’ Kwa kanuni hiyo jiwe litaendelea kubaki lilipo kama hakuna kitu chochote kitakacholigusa au kulitingishwa. Kumbe kama unataka mabadiliko yoyote katika nyanja yoyote ya maisha yako huna budi kufanya mabadiliko. Yafuatayo ni mabadiliki yaliyobeba siri ya maotokeo uliyoyasubiri kwa siku nyingi;
Amsha kilicholala. Ndani yako kuna uwezo wa kipekee wa kukuwezesha kufanya kitu cha pekee na kupata chochote unachotaka kam utajiri, umaarufu, mahusiano mazuri nk. Lakini unaweza kujiuluza kama unauwezo huo kwa nini sasa hupati vitu hivyo? Ni kwa sababu uwezo huo bado umelala tu. Uhahitaji kufanya mabadiliko ya kuuamusha uwezo huo uliolala kwa kuwa na ndoto kubwa na kuweka malengo makubwa.
Mtaji uwe biashara. Umekuwa na mtaji siku nyingi lakini huanzishi biashara ambayo ungeweza kuikuza kwa na kupata utajiri. Inawezekana mtaji huo unao mkononi na kila siku unajiuliza nifanye biashara gani. Ili uweze kuwa na biashara yenye mafanikio unahitaji sasa kutengeneza wazo la biashara kutoka kwenye vitu unavyovipenda na kuanza kutoa thamani. Mtaji huo utakupa faida na kuzaa zaidi.
Uvivu kuwa kazi. Umekuwa unapanga mipango mizuri ya kufanyia kazi lakini uvivu unakuingia, unatekeleza kidogo au hutekelezi kabisa. Hakuna matokeo unayoweza kupata kwa kuwa na mipango pekee, ni lazima uweke kati kwanza. Jisukume kufanya mabadiliko haya, acha uvivu weka kazi.
Kuahirisha kuwa nidhamu. Kuahirisha mambo kimekuwa ni kikwazo kikubwa cha watu kutopata matokeo. Nitafanya kesho, umekuwa wimbi wa watu wengi. Fanya mabadiliko sasa, muda mzuri wa kufanya kile unachotakiwa kufanya ni leo tena sasa, usiseme kesho, haipo.
Chuki kuwa upendo. Maisha ya binadamu yanathiriwa sana na hisia hizi mbili; chuki na upendo. Ili mahusiano yako binafsi na watu wengine yawe mazuri huna budi kufanya mabadilko haya; tawaliwa na upendo na sio na chuki. Hili linawezekana kwa kuwachukualia na kuwasamehe wengine.
Ndugu! Kitu gani umekuwa ukikisubiri kwa muda mrefu kitokee maishani mwako, je ni utajiri? Furaha? Umaarufu? Ridhiko au nini? Hivyo vyote vitapatikana kwa kufanya mabailiko. Na hii ndiyo siri ya kupata matokeo ya mafanikio. Fikiri mifano ya mabadiliko hapo juu kisha anza kufanya mabadiliko ili kupata matokeo ya utofauti.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz