Kama Unafanya Hivi Kuwa Na Uhakika Wa Kutofika Safari Yako.


Categories :




“Njia pekee ya kuwa na uhakika wa kutojikwaa ni kutotembea. Lakini kutotembea ni uhakika wa kutofika”

Ni wazi kuwa unapotembea na hasa nje unaongeza hatari ya kujikwaa kuliko yule anayeamua kubaki ndani. Lakini anayebaki ndani hawezi kupata kitu kingine chochote zaidi ya vile alivyonavyo pale alipojifungia. Pia hawezi kwenda sehemu nyingine yoyote bali kubaki mazingira hayohayo. Lakini wapo ambao hawataki kujikwaa na hivyo huamua kubaki ndani.

Inawezekana na wewe ni miongoni mwa watu hao ambao wamekuwa wakijfungia ndani bila kutoka nje na kutembea kwa hofu ya kujikwaa. Au mara nyingine umetoka nje lakini ukaishia kuzunguka palepale nyumbani kwako una uhakika unapofahamu na hutaweza kujikwaa.

Unaweza ukjiuliza ni lini umefanya mambo kama haya? Mbona kila siku naondoka nyumbani na kufanya shughuli zangu? Ndugu! Kwa kuogopa kufanya vitu vipya umeamua kujifungia ndani na kuendelea kufanya mambo yaleyale uliyoyazoea ni kuamua kujifungia ndani ili usijikwae.

Ni mara ngapi umekutana na fursa ambayo uliona ndiyo inabidi uifanye ili uweze kukua zaidi ya ulipo, ila woga wa kutokuwa na uhakika wa kutopata matokeo uliyoyatamani ukakuingia kisha ukaamua usifanya jambo hilo? Ni jambo gani umeendelea kufanya vilevile licha ya kupata matokeo ambayo hayakuridhishi lakini hujataka kubadili mbinu kwa sababu tu utaanza kufanya vitu ambavyo hujazoea? Ndugu! Huu ni uhakika kuwa kutofika safari yako.

Kuna safari ya mafanikio unayotamani uifikie kama kuwa vile kuwa na biashara yenye mfanikio, kuwa tajiri, kuwa kiongozi fulani mkubwa, kujilikana na mtu wa thamani kubwa jamii. Haya yote hayatatokea kama hutaamua kutoka hapo ulipo kwa kujizuia usipata maumivu. Ili uweze kufika safari yako ya mafanikio ambayo mara nyingi ni ndefu na yenye maumivu makali huna budi kutoka nje.

Toka nje kwa kuwa tayari kufanya vitu ambavyo hujawahi kuvifanya. Umekuwa ukipendelea kufanya vitu ambavyo una uhakika wa kupata matokeo hata kama kwa kiwango kidogo kuliko unachotarajia. Sasa panga mipango ya kuapata matokeo makubwa unayostahili na kubali kuanza kufanya huko ukingalia ni hatari gani unaweza kuzipata na namna ya kuzipunguza.

Jenga uvumilivu. Kwa ajili ya kuanza kufanya vitu vikubwa na ambavyo umekuwa huvifanyi kun uwezekano wa kupata matokeo ambayo hujazoea. Njia pekee ya kukabiliana ni kuwa mvumilivu, pale unapopata matokeo usiyotarajia, usiache bali jifunze wapi kwa kuboresha kisha songa mbele.

Ndugu usikubali kuwa na uhakika wa kutopata matokeo kwa kuendelea kujifungia ndani ya mazoea. Wakati umefika sasa wa kutoka nje kwa kufanya vitu vya utofquti na sahihi. Hata kama hutapata matokeo mara moja, vumilia kama upo kwenye sahihi kufika ni lazima.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *