Utajiri Wako Umejificha Hapa.


Categories :

“Utajiri wa umaarufu wa nyuki haujabebwa na uzuri wa umbo lake bali kile anachoweza kukitengeneza”

Kila mwanadamu anatamani kuwa tajiri. Mahangaiko mengi ya maishanya mwanadamu yanalenga kupata utajiri kila eneo la maisha yake. Utajiri wa mali au fedha ndiyo hutawala vichwa vya watu wengi.

Licha ya jitihada hizo ambazo wanadamu wengi hawapati utajiri ule wanaotamani. Ni idadi ndogo sana ya watu hufikia utajiri huo. Hivyo unaweza kujiuliza utajiri huo umejificha wapi? Nini siri ya utajiri huo? Kitu gani matajiri wanakifanya ambacho masikini au watu wa kawaida hawakifanyi?

Leo ifahamu siri hii kuu ya utajiri na wewe iishi ili uweze kupata utajiri katika eneo lolote la maisha yako. Siri hii ni kuwa utajiri umejificha kwenye THAMANI. Chanzo kikuu cha utajiri wako ni thamani. Thamani ni kitu chochote iwe bidhaa au huduma unayotoa kwa watu wengine na kuwasaidia kutatua changamoto zao.

Kwenye biashara yako lazima wateja wako waione thamani ndipo waweze kupatia fedha. Kuna nguvu kubwa sana ya uvutano iliyopo kati ya mtu na fedha yake na hivyo hawezi kuiachia fedha yake kirahisi. Nini kitaivunja nguvu hiyo ni THAMANI.

Kazini kwako, lazima boss wako aione thamani unayoitoa kila siku ili aone sababu ya wewe kuendelea kuwepo kwenye ofisi yake. Thamani ambayo utaendelea kuitoa itaendelea kutoa matokeo ambayo yatamshawishi boss wako kukipandisha cheo chako au kukuongezea mashahara. Thamani gani unatoa kazini kwako?

Ili watu wakulipe ni lazima kuwe tayari na thamani unayoitoa. Hutapata fedha kwa sababu upo duniani na una uhitaji mkubwa sana fedha, wala hutapata fedha kwa sababu uso wako unatia huruma sana na hivyo dunia itakuonea huruma la hasha! Bali watu watakuwa tayari kukulipa fedha kwa sababu ya thamani unayowapa.

Katika historia tunaambiwa kulikuwa na biashra ya mabadilishano iliyotambulika kwa jina la “burter trade” hii ilikuwa ni biashara ya kubadilishana vitu moja kwa moja. Unanipa mahindi nakupa mbuzi , unanipa shoka nakupa cahakula nk. Hivi ndiyo ilivyo kwenye utajiri, unatoa thamani kubwa kisha dunia inakupa utajiri.

Mafanikio uliyapata nia matokeo ya thamani uliyowapa watu wengine. Kama umepata mafanikio kiduchu, tambua kuwa hata thamani unayowapa watu wengine ni kiduchu hivo hivyo. Ili uweze kufikia utele/utajiri kwenye kila unachokifanya, hakikisha unatatua matatizo ya watu wengine kiasi cha wao kuwa tayari kukulipa kukilipa kiasi kikubwa cha fedha cha kukufikisha kwenye utajiri.

Kazi kubwa ambayo muda mwingi inabidi uifanye kwenye biashara unayofanya ni kuongeza thamani yake kila siku. Kila siku ongeza thamani ya hudumia kwa wateja waone kweli wao ni wafalme. Kila siku ongeza ubora na upekee wa bidhaa au huduma yako ili watu wasifikirie kuondoka na kutafuta mbadala. Panua biashara huku ukilinda ubora hapo ndipo utapata malipo zaidi kutoka kwa watu wengine.

Utajiri wa nyuki upo kwenye thamani ya asali anayoitengeneza. Utajiri wako utoke wapi?

Ndugu! Hii ndiyo siri ya utajiri ambayo na wewe unaweza kuiishi na kufanikiwa kupata utajiri huo ambao umeutamani siku nyingi bila mafanikio. Kila mtu anayetaka mafanikio maishani mwake anafanya biashara. Anza leo kuongeza thamani ya biashara yako katika maeneo mbalimbali, kadri utakavyongeza thamani kwa watu ndivyo watakapokuwa tayari kukulipa zaidi na hivyo wewe kufikia utajiri.

Chukua hatua: Angalia maeneo mablimbali ya biashara yako kisha panga kuanza kuongeza thamani kwenye kila eneo la biashara yako. Panga kutorudi nyuma katika hili ili kadri thamani yako itakavyokuwa inaongezeka kwao watakuwa radhi kukulipa zaidi.

Kuongeza thamani ni kuukaribia utajiri.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *