Dawa Ya Kwanza Kabisa Ya Kutibu Ugonjwa Wako Wa Kushindwa.
Ugonjwa ni hali ya kutokuwa sawa ndani ya mwili wa mtu. Hii ni hali ambayo inakifanya viungo au mfumo fulani kutokufanya kazi kwa ushihi. Kiungo hicho kisipofanya kazi kwa usahihi, huathiri na viungo vingine kutokufanya vizuri pia.
Mtu huanza kusikilizia dalili pale ugonjwa unapokuwa ndani yake. Dalili mojawapo ni maumivu, homa, kuishiwa nguvu nk. Hapo ndipo mtu humlazika kwenda kumuona daktari ili kupata matibabu kwa ajili ya ugonjwa wake.
Upo ugonjwa mwingine zaidi ya ule wa mwili, huu ni ugonjwa wa kushindwa. Huu ni ugonjwa unaowatesa watu wengi. Watu wengi wana dalili za ugonjwa huu lakini bahati mbaya ni hii kuwa wengi hawajapata dawa tofauti na wengi walivyopata dawa ya kutibu malaria na kupona.
Ili uweze kutibu ugonjwa wowote wa mwili kwa mafanikio makubwa huna budi kujua kisababishi au visababishi vya ugonjwa huo. Vinginevyo ukiishia kutibu dalili tu, itakuwa ni vigumu kwa ugonjwa huo kutoweka. Vivo hivyo ili uweze kutibu vyema ugonjwa wa kushindwa katika maisha huna budi kutambua kisababishi cha kushindwa.
Sababu kubwa inayosababisha ugonjwa wa kushindwa maishani mwako ni mtazamo. Hii ni namna unavyoviona vitu na hivyo kuathiri maamuzi unayoyachukua. Ni mtazamo sahihi tu ndio unakufanya uchukuae hatua sahihi za kukufanya ufanikiwe kwenye jambo lolote.
Una mtazamo gani kuhusu maarifa? Ukisikia kuhusu maarifa unapata picha gani? Je unaona maarifa yana umuhimu wowote kwenye mafanikio yako? Kama una mtazamo hasi kwenye maarifa ukiamini kuwa maarifa hayana mchango wowote kwenye mafaniko zaidi ya kazi tu, huwezi kuyatumia na yakakupa mafanikio?
Una mtazamo gani kuhusu utajiri ina nguvu kubwa sana wewe kupata au kuukosa utajiri. Je unafikiri utajiri ni bahati tu, na wachache wanayo bahati hiyo au na wewe kuna siku utapata bahati hiyo? Je unaona utajiri ni mbaya na matajiri wote ni watu wabaya?
Mtazamo wako juu ya jambo unaweza kuwa chanya aua hasi. Unapoona utajiri ni mbaya huu ni mtazamo chanya na pale utakapoona ni mbaya unakuwa kwenye upande hasi. Nini utafanya itategemeana na mtazamo wako. Kama huna mtazamo sahihi juu ya kupata utajiri, kwa mfano kwa kuamini kuwa utajiri ni bahati tu, basi utaendelea kukaa tu bila ya kuweka mikakati yoyote ukisubiri siku ifike na wewe ubahatike.
Huwezi kubadili hali yako ya kushindwa na kuwa na mafanikio mpaka pale utakapotibu ugonjwa huu wa mtazamo. Usipotibu mtazamo wako, utaendelea kuhangaika na dalili za kushindwa bila mabadiliko yoyote chanya. Hivyo dosi ya kwanza ya kutibu kushindwa kwako ni ya kubadili mtazamo wako. Na dosi hii itibu vifuatavyo;
Mimi siwezi. Huu ni mtazamo hasi unaohitaji dawa ili upone. Utakapopona utajiona unaweza. Watu wengi wameshindwa kupiga hatua kwa sababu tu ya kujiona hawawezi, wakiamini ni watu fulani tu wenye uwezo wa kupata mafanikio. Kila mtu ana uwezo mkubwa ndani yake wa kufanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na wewe. Anza kuamini kuwa unaweza; utakuwa mwanzo mzuri wa kuanza kupiga hatua.
Sina bahati. Kila mtu ana bahati, lakini itamfikia pale atakapokuwa anafanya vitu. Mwanafalsa Seneca alisema “Luck Is What Happens When Preparation Meets Opportunity” ikiwa na tafsiri kuwa bahati huja pale maandalizi yanapokutana na fursa. Kumbe ni lazima uwe unafanya kitu fulani ndipo utakutana na bahati. Huwezi kupata bahati ukiwa umekaa tu hufanyi kitu chochote.
Mimi ni mshindi. Huwezi kuendelea kupigana vita kama akili yako inaona kushindwa mbele yako. Kupata mafanikio ni vita dhidi ya vikwanzo mbalimbali vinavyosimama kwenye barabara ya mafanikio. Je unaona ukiwa umepata mafanikio licha ya changamoto kubwa unazokutana nazo? Ukiwa na mtazamo wa ushindi utaendelea kuchukua hatua licha ya changamoto unazokutana nazo. Lakini itakuwa ni ngumu kwako kuendelea kung’ang’ania hatua za mafanikio kama huuoni ushindi.
Mhimili huu wa mtazamo ni mmoja kati ya mihimili kumi na mbili iliyoelezewa kwa kina kwenye kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Nina imani wewe ni miongoni mwa watu wanaotaka kujenga mafanikio makubwa na ya kudumu, hivyo nakushauri usikose kupata nakala ya kitabu hiki ili upate mwongozo sahihi wa kuwafikia mafanikio hayo.
Gharama ya kitabu hiki ni Sh 20,000/ lakini kwa sababu najali mafanikio yako, sasa utakipata kwa sh 15,000/ tu. Wahi kabla ya ofa hii kuisha. Wasiliana nami kupitia namba 0752 206 899(Alfred Mwanyika).
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.t