Dawa Ya Tatu Ya Kutibu Ugonjwa Wako Wa Kushindwa.
Kama ulihudhulia kliniki ya makala mbili zilizopita, mpaka sasa utakuwa umepokea dawa mbili za ugonjwa wako wa kushindwa. Dawa ya kwanza ilikuwa ni ya kubadili mtazamo na ya pili ilikuwa ni ya kuweka malengo. Kama hukupata bahati ya dawa hizo mbili za kwanza, unaweza kujipatia bure kabisa kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini; dawa ya kwanza https://www.amshauwezo.co.tz/wp-admin/post.php?post=1180&action=edit na ya pili https://www.amshauwezo.co.tz/wp-admin/post.php?post=1185&action=edit
Leo nitakushirilisha dawa ya tatu ambayo unahitaji ili uweze kupona ugonjwa wako wa kushindwa. Kwa dawa dawa mbili zilizopita unaweza kuanza kupata nafuu lakini unahitaji dawa nyingine ya tatu katika mwendelezo wa kupona ugonjwa wako wa kushindwa. Dawa hiyo ya tatu ni kazi.
Kubadili mtazamo kutakusaidia kutambua kitu sahihi kwako kukifanya. Kuweka malengo bora yatakusaidia wewe kutambua mwelekeo sahihi wa kuweka nguvu na umakini wako lakini pia wapi utumie muda wako. Lakini hata kama utakuwa na melengo bora kiasi gani, usipoweka kazi hakuna matokeo unayoweza kupata.
Kutokuweka kazi kimekuwa kisababishi kikubwa cha watu wengi kutokupata matokeo licha ya kuyatamani sana mafanikio. Hii ni sababu ya watu wengi kuugua ugonjwa huu wa kushindwa.
Ndugu! Hakuna kinachoweza kutokea maishani mwako bila kuweka kazi. Kama kweli umeweka malengo yako vizuri, kitu pekee kitakachokulipa kwenye malengo yako ni kazi. Watu wengi hawafanikiwi kwa sababu hawapendi kazi. Kazi ninayozungumzia hapa sio ile ya kugusa gusa tu bali kuweka nguvu, umakini na muda wako kwenye jambo moja uliloamua kulifanya mpaka upate matokeo.
Kazi ni rafiki wa kweli. Kuna marafiki wengi umeshawahi kuwa nao maishani, lakini wengine mlishasahauliana, walishafariki, hamuaminiani na mmesalitiana nk. Lakini kazi ni rafiki wa kweli. Huwezi ukaungana naye akakusaliti. Kila anayetengeneza uadui na kazi huishia kuugua ugonjwa wa kushindwa. Weka urafiki na kazi.
Usishindwe kwenye kazi. Unaweza ukakubali watu wakushinde kwenye uzuri, mabishano, mipango, nk lakini usikubali wakushinde kwenye kazi. Ukiwa mshindi kwenye kazi, utakuwa mshindi kwenye maisha yako.
Mwili wako usikudanganye. Kati ya kitu ambacho mwili wako huwa haupendi ni kuufanyisha kazi. Ndiyo maana hata baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi unaanza kujisikia kuchoka. Hii ni kwa sababu miili yetu ina uvivu wa asili. Huwa inapenda sana kutunza nguvu. Hii ni kutokana historia ya hapo zamani kuwa kwenye mazingira hatarishi hivyo ilijitengenezea utaratibu wa kutunza nguvu kwa ajili ya kutumia kwenye dharura kama za wanyama wakali. Tafiti zinaonyesha kuwa hata pale unapojiona mwili umechoka sana na huwezi kuendelea kufanya kazi, unakuwa umetumia 40% tu ya nguvu zako. Hivyo usikubali kudanganywa na mwili wako, hata pale unahisi kuchoka unaweza kuendelea kuamsha nguvu zako kwa kuuambia mwili wako unanidanganya.
Hii ni Habari Njema Kwako!
Ndugu yangu, hii ni nguzo mojawapo kati ya nguzo 12 za kujenga mafanikio zilizoelezewa kwenye kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Nguzo nyingine ni kama kutambua uwezo wako wa kipekee, kujenga ndoto yako kubwa, kujenga nidhamu, ustahimilivu na ung’ang’anizi nk
Hiki ni kitabu cha kuhakikisha unakipata kama kweli una nia ya kujenga na kulinda mafanikio makubwa. Gharama ya kitabu hiki ni Sh 20,000/ lakini kwa sababu najali mafanikio yako, sasa utakipata kwa sh 15,000/ tu. Wahi kabla ya ofa hii kuisha. Wasiliana nami kupitia namba 0752 206 899(Alfred Mwanyika).
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz