Hivi Ndivyo Unavyoweza Kufurahia Kifo Jioni Baada Ya Kuzaliwa Asubuhi.
Kifo jioni! Hili linawezekana kuwa limekushitua sana baada ya kupata picha kuwa inabidi uzaliwe asubuhi kisha ufe jioni. Maisha ya binadamu yoyote yana matukio mawili muhimu, moja ni kuzaliwa ambao ni mwanzo na jingine ni kufa ambao ndiyo mwisho.
Uhai wako ndiyo maisha yako. Jana ni muda ambao umekwishapita. Hutaupata tena muda kama huu. Huwezi kufanya kitu chochote jana. Kesho inasemekana ni muda mwingine lakini ni muda ambao huna uhakika nao kama utafika huko au la. Hivyo umebakiwa na leo tu ambayo upo. Hivyo maisha yako ya uhakika yapo kwenye siku ya leo.
Kwenye ya LEO ambayo una uhakika nayo ina asubuhi ambapo unaamuka na jioni au usiku unapoenda kulala. Ukishalala kisha kuamka unakutana na leo nyingine. Hii ina maana unazaliwa asubuhi na kisha kufa jioni huku ukisubiri bahati ya kuzaliwa tena leo ya kesho.
Mtazamo huu ni muhimu sana katika kuishi maisha yako kikamilifu. Usipofanya hivyo kuna nafasi ya kuendelea kuiishi jana ingali imeshapita na huwezi kugeuza chochote ambacho ulishakifanya jana. Wapo watu wanaoendelea kujutia yale waliyokosa jana kiasi cha kushindwa kuweka umakini kwenye siku ya leo. Wapo amabo wanaiishi kesho kwa hofu kubwa kwa sababu hawana uhakika wa kile kinachokwenda kutokea.
Kumbe siku yenye thamani kubwa sana na inayoamua maisha yako ni leo. Unazaliwa asubuhi kwa sababu hapo ndipo unapoaanza siku yako njema. Unakufa jioni kwa sababu ndiyo unaimaliza siku ukisubiri kama utabahatika leo nyingine.
Ili uweze kufurahia kifo chako jioni huna budi kuanza kujipanga tangu unapozaliwa asubuhi. Hakikisha umeipangilia siku yako vizuri huku ukijua kwa dhati kabisa ni kitu gani unaenda kufanya na muda gani. Fanya vifuatavyo ili uweze kufurahia kifo chako jioni;
Vipaombele. Kuna vitu vingi vinavyoweza kuwa mbele yako na ukatamani kuvifanya. Lakini wewe anza na kile ambacho ni cha thamani sana mbele zako kiasi kwamba hutapenda ufe jioni kabla hujakifanya hicho. Hicho kiwe cha kwanza na kifanye kwa ustadi mkubwa.
Nidhamu Kali. Utakifurahia kifo chako jioni kama utaiendea siku yako kwa nidhamu ya hali ya juu sana. Hiki ni kitendo cha kutosikiliza sababu yoyote kwenye kukamilisha jambo ulilopanga kulifanya. Nidhamu hii ni pamoja na kujilazimisha kufanya hata pale ambapo hujisikii.
Kila siku iwe mpya kwako. Mmoja ya sababu ya watu kutoiishi siku kikamilifu ni kuridhika na kile alichokwisha kukipata. Kipato ulichokipata, wateja wengi uliowapata, nk visikutanye usiweke nguvu siku hii ya leo.
Nina Habari Njema Kwako!
Kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO ni mwongozo sahihi wa kukufanya ufurahie kifo chako kila jioni ikifika. Kitabu hiki kina DONDOO 366 na hivyo kukuwezesha kusoma dondoo moja kila siku kwa mwaka mzima na kuufanya mwaka mzima kuwa wa mafaniko.
Hizi ni dondoo zinazojenga mihimili 12 ya mafanikio yako kama kutambua nguvu ya kipee uliyonayo, kutambua ndoto yako na kuweka malengo, kazi na nidhamu, kutoa thamani nk. Jipatie nakala yako leo ili uanze kuiishi siku kwa mafanikio na kisha kufurahia kifo chako.
Gharama ya kitabu hiki ni Sh 20,000/ lakini kwa sababu najali mafanikio yako, sasa utakipata kwa sh 15,000/ tu. Wahi kabla ya ofa hii kuisha. Wasiliana nami kupitia namba 0752 206 899(Alfred Mwanyika).
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz