Haya Ndiyo Macho Ya Kukufikisha Unakostahili Kufika.
Tangu umezaliwa mpaka sana, ni muda mrefu umepita. Kuna sehemu umekuwa ukiwaona watu wamefika unabaki unashangaa wamefikaje huko!
Kuna mambo makubwa watu wameyafanya, unashangaa wamewezaje! Unajaribu kufanya lakini hufiki mbali, unajiuliza tatizo ni nini? Mara nyingine ukahitimisha kuwa hao waliofanya mak uh bwa wamependelewa.
Kuna kitu kimekuwa kikikosekana kwako ndiyo maana umeshindwa unakotakiwa ufike. Watu wengi wamekufa wakiwa hawajafika sehemu wakizotakiwa wafike. Yaani wameshindwa kupata mafanikio makubwa waliyosathili. Kitu hicho unachokikosa ni macho ya kuona na kukufikisha unakotakiwa kufika.
Ili uweze kufika unakotakiwa kufika, unahitaji macho zaidi ya haya ya nyanya yaliyo usoni kwako. Unahitaji macho yanayoweza kuona mbali zaidi. Unahitaji macho yanayoweza kuona picha kubwa zaidi ya macho haya ya nyama. Unahitaji macho yanayoweza kuona mwaka kesho, miaka 5,10,20 hata 50 ijayo. Haya ni macho ya akili yakiunganishwa na moyo.
Ukilinganisha uwezo kuona kati ya bundi na binadamu, bundi anaweza kuona mara kumi au zaidi ya binadamu. Lakini kwa kutumia macho ya ndani ya akili ilichonganyika na imani ya moyo, binadamu anaweza kujenga picha kubwa sana ndani yake na anaweza kufika mbali mara dufu ya bundi.
Kumbe njia pekee ya kufika unakostahili kufika ni kutumia akili na moyo wako kuona kwanza unakotakiwa kufika na kuanza safari hiyo kwa imani. Huko unakotakiwa kufika na yale unayotarajia kuyapata huitwa maono.
Unahitaji kuwa na maono ili kuacha kutegemea macho ya nyama pekee. Macho haya ya nyama hayatakufikisha mbali kwani;
Yanaona vichache tu. Usifanye tu vinavyokujia muda huo, bali jenga maono kwenye macho yako ya ndani inayoweza kuoana vitu vingi kwa wakati mmoja.
Yanaona sasa tu. Wakati macho yanaona vilivyopo muda huo, unahitaji akili ya ndani inayoweza kuona miaka kumi, hata hamsini ijayo. Huko ndiko kwenye makuu unakotakiwa kufika.
Kukatisha tamaa; Macho ya nyama yanona vikwazo vingi na yanakosa imani kubwa ya kuendelea kuchukua hatua pale yanapokutana na changamoto kisha kujata tamaa. Akili yako ya ndani inaona maono. Macho haya ya ndani yanaona mwisho tangu mwanzo hivyo hata kama changamoto zitasimama njia yanazidi kuweka juhudi yakiamini vikwazo hivyo ni vya muda tu.
Ndugu! Kuishi kwa kufanya jambo lolote unaloliona ndiyo kumekufanya kuwa mtu wa kawaida. Wakati umefika sasa wa kuanza kutumia macho ya ndani kwa kuwa na maono.
Kitu gani kikubwa unatamani ukipate au ukifanye kipindi cha uhai wako hapa duniani? Jenga picha hiyo ndani yako kisha weka mipango ya kuanza kuivuta kwenye uhalisia. Mtu yoyote akikuambia huwezi kutimiza maono hayo, usimusikilize kwani yeye anaangalia kwa macho ya nyama. Maono gani unayo kwenye maisha yako.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz