Hivi Ndiyo Viashiria Vya Kujua Kama Unakua.


Categories :

Zimebaki siku chache tu niuage mwaka huu na kuuakaribisha mwaka mwingine mpya. Itakuwa bye bye 2022 na karibu 2023.

Haya ni mawazo ambayo yapo kwenye vichwa vya watu wengi ikiwa ni mwisho wa mwaka huu ambao unaonekana ulianza juzi tu. Inawezekana na wewe ni miongoni mwa watu wanaosubiria kwa hamu kuhamia mwaka mwingine.

Kubadilika kwa mwaka ni kiashiria kwamba muda wa dunia hii unazidi kukua. Muda hausimami, unakua tu. Ili kuwa na maisha yenye mafanikio hapa duniani, unatarjiwa na wewe kukua kama ambavyo muda wa dunia hii unakua?

Kitu chochote kisichokua kinakufa, ni suala la muda tu. Kama biashara yako haikui, itakufa ni suala muda tu. Kama fikra zako zako hazikui zinakufa nk

Unaweza ukawa unajiuliza uatajuaje kama unakua au la? Mtoto akienda kliniki anatarajiwa uzito wake uwe mkubwa kulilo wa awali. Isipotokea hivyo, mzazi na mhudumu atashangaa. Mbegu ya mhindi ikipandwa inatarajiwa imee na kuanza kukua kufikia mhindi mwingine mkubwa isipofanya hivyo mpanzi atashangaa. Kumbe kigezo kikuu cha ukuaji ni mabadiliko.

Unajua kama unakua endapo utayaona mabadiliko chanya katika maisha yako. Kama huyaoni mabadilko chanya kwenye eneo unalofikiri unakua, basi tambua umedumaa na unahitaji virutubisho kuanza kukua. Vifuatavyo ni baadhi ya viashiria muhimu vya ukuaji wako.

Thamani yako inaongezeka. Kila aliyopo hapa duniana ana thamani kwa watu wengine. Una kitu cha pekee cha kuipa dunia. Je idadi ya watu wanafaidika na thamani yako inazidi kuongezeka?

Kipato kuongezeka. Kama thamani yako inaongezeka na kipato chako pia lazima kiwe kinaongezeka? Je ukilinganisha kipato chako mwanzoni kwa mwaka na sasa ni tofauti, kama kipo pale pale , ina maanisha unadumaa.

Uelewa kuongezeka. Kitu gani kipya unakielewa tofauti na mwanzoni? Je kuna taaluma gani ambayo umeiongeza kwa mwaka huu? Kama unaendelea kufanya vitu vyaka kama ulivyokuwa unafanya Januari, basi tambua hujakua.

Uvumilivu kuongezeka. Magumu yanapokujia unachukua hatua gani? Majibu yanapochelewa unachukua hatua gani? Watu wanapokukatisha tamaa unafanya nini? Je uvumilivu wako wa kuzikabili changamoto umeongezeka? Au bado vile vile, ukikutana na ugumu unarudi nyuma?

Wateja wanaongezeka. Unafanya biashara na unatamani ikue! Je kuna ongezeko la wateja wangapi sasa ukilinganish na Januari? Kama hakuna au ni kidogo sana basi tambua kuwa hukui.

Ushawishi unaongezeka. Ushawishi unakufanya watu wafuate kama kiongozi. Ushawishi unakufanya wateja wengi unaokutana nao wanunue. Ushawishi unaboresha mahusiano. Ushawishi wako umeongezeka kwa kiasi gani?

Ndugu! Hivi ni baadhi ya viashiria muhimu kukuonyesha kama unakua au unadumaa na kufa kabisa. Kaa chini na jipime na kila kiashiria hapo juu ili uweze kuupangilia mwaka wako mpya 2023 na kuwa mwaka wa ukuaji mkubwa kwako.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *