Ni Mpaka Uviweze Hivi Vidogo Kwanza!
Ndugu yangu, najua unatamani vitu vikubwa kwenye maisha yako. Ni kweli una haki ya kuvipata. Lakini kama hujavipata, kuna vitu vinavyokuzuia.
Kuna vitu vinavyokuzuia usipate vitu vikubwa. Vitu hivyo vinaitwa vitu vidogo. Kumbuka hata vitu vikubwa vinaanza na udogo wake. Wanasema safari ya maili elfu moja inaanza na hatua moja.
Dhana ya kukitaka kitu na kuona ni lazima uanze kwa ukubwa wake ndicho kilichowafanya watu wengi kutopata vitu hivyo vikubwa.
Unatamani uwe mfanyabiashara mkubwa,lakini hutaki kuanza na biashara ndogo, ukifikiri kuna siku utaanza na biashara hiyo ya ndoto yako kwa ukubwa huo.
Unatamani kuwa mtu fulani maarufu, lakini hutaki kuanza kujulikana na watu wachache kwanza wanaokuznguka ukifikiri siku utaamuka asubuhi na kuwa maarufu.
Vitu vidogo ndivyo vinavyokuzuia kufikia ukubwa wako. Ni mpaka pale utakapokuwa mwaminifu kwenye vidogo ndipo utapata.
Vifuatavyo ni vitu vidogo ambavyo ukivifanya kwa uaminifu utafanikiwa kufanya na kupata matokeo makubwa.
Kipato kidogo. Ni muda mrefu sasa umekuwa ukikipata kipato kidogo kutokana na biashara/ huduma au ajira unayoifanya. Umekitumiaje kipato hicho? Kwa nini hakikui? Huwezi kupata kipato kikubwa kama hicho kidogo umeshindwa kukikuza.
Hata kidogo unachokipata kitumie kama mtaji wa kukuza zaidi.
Biashara ndogo uliyonayo. Ni muda gani umepita tangu ulivyoianzisha biashara yako? Kama biashara yako imebaki kwenye udogo ule ule licha ya muda mrefu kupita, tambua hicho ni kikwazo kikubwa cha wewe kufanya makubwa. Anza biashara kwenye udogo, lakini endelea kuikuza biashara yako kwa kuwafikia wateja wengi zaidi.
Mafanikio uliyoyapata. Ulijisikiaje baada ya kupata mafanikio fulani ambayo umeyakumbatia mpaka sasa? Ilikuwa ni haki yako kufurahia kile ulichokipata. Lakini hakitakiwi kuwa ndiyo kufuli la kukufungia mafanikio yako makubwa zaidi. Licha ya ukubwa wa mafanikio uliyoyapata, kama hutakuwa zaidi ya hapo basi utaanza kufa. Mafanikio yako ya sasa yanapaswa kuwa ni ngazi ya kupata makubwa zaidi.
Kuweka akiba ndogo. Kuweka akiba ni nidhamu. Nidhamu hii inaanzia kwenye kipato kidogo. Utafanikiwa kuwa na mtaji mkubwa na kisha kuuwekeza zaidi kama utafanikiwa kujenga tabia hii ya kuweka akiba hata sasa wakati una kipato kidogo. Kama sasa huweki akiba usijifariji kuwa kipato kikiongeza ndiyo utakuwa unaweka akiba.
Ndugu! Ni habari njema kwako. Kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO kinakusaidia kujenga nidhamu ya kufanya kitu kwa udogo lakini kila siku.
Hiki ni kitabu kinachokujengea nguzo 12 za mafanikio ya maisha yako kama kutengeneza maono na malengo, nidhamu na kazi, ustahimilivu, thamani na utajiri nk kwa kusoma DONDOO 1 kila siku kwa mwaka mzima bila kujirudia.
Pata picha ukubwa wa maarifa na mafanikio utakuwa nayo tar 31 Disemba 2023 baada ya kufanikiwa kusoma DONDOO 365 na kuzifanyia kazi. Hakika hutakuwa kama ulivyo sasa. Utakuwa umekua sana.
Gharama ya kitabu hiki ni sh. 20,000/ lakini kipate leo kwa bei ya ofa sh 15,000/. Uufanye mwaka 2023 kuwa wa kufanya vitu vidogo kwa nidhamu ili kupata vikubwa.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz