Hiki Ndicho Kinaishinda Elimu Na Kipaji .
Ningekuwa nina elimu kubwa kama elimu ya chuo, ningefika mbali sana. Ningekuwa na kipaji kama mtu fulani ningepiga hatua kubwa sana maishani mwangu.
Ndugu wapo wenye elimu kubwa hata za vyuo vikuu lakini hawana mafanikio makubwa wanayostahili. Kuthibitisha hilo, fanya uchunguzi, matajiri wengi duniani na nchini kwako hawana elimu kubwa unaozifikiri zingekusaidia kupata utajiri.
Kadhalika kili mtu ana kipaji, lakini hata wale waliofanikiwa kuvigundua vipaji vyao wengi wameishia kuwa watu wa kawaida. Hii ni ishara kuwa kuna kitu ambacho ni zaidi ya elimu na kipaji kinachomwezesha mtu kutikia mafanikio makubwa anayostahili.
Leo unaenda kukifahamu kitu hicho kinachozidi elimu na kipaji ili na wewe ukitumie kupata mafaniko makubwa. Kitu hicho ni UVUMILIVU.
[ ] Kuvumilia ni kuendelea kufanya bila kujali ugumu unaokutana nao
[ ] Uvumilivu ni kuendelea kufanya hata kama matokeo yanachelewa
[ ] Uvumilivu ni kupita njia sahihi ndefu hata kama kuna njia fupi isiyo sahihi ipo
[ ] Uvumilivu ni kutoa neno haiwezekani maishani mwako
Baada ya mtu kutambua kile anachotaka kukipata maishani na kisha kuwa tayari kulipa gharama za mafanikio hayo, anachohitaji ili kupata mafanikio yake ni Uvumilivu.
Lakini uvumilivu unabebwa na kitu kinachoitwa NIDHAMU. Hiki ni kichocheo kikubwa sana cha mafanikio yako. Ndihamu ni kufanya kilicho sahihi bila kuruhusu sababu yoyote ile ikuzuie. Huku ni kufanya bila kujali unajisikia au hujisikii. Huku ni kufanya bila kujali ugumu unaokutana nao.
Watu wengi wanafahamu kipi sahihi cha kufanya, lakini hawafanyi. Wenye elimu kubwa na vipaji wanaweza kufahamu nini wanchotakiwa wakifanye ili waweze kupiga hatua kubwa katika maisha yao, lakini hawafanyi hivyo. Wapo wanaojaribu kufanya lakini si kwa msimamo. Muda ambao wanakuwa hawajisikii, hawafanyi.
Lazima ujenge nidhamu kali maishani mwako kukuwezesha kuvumilia pale unapoanza kuifanyia kazi mipango yako. Vizuizi au changamoto haviogopi mipango mizuri uliyonayo bali uvumilivu utakaoweka kwenye kile unachofanya.
Ndugu! Bila kujali elimu uliyonayo au kipaji ulichonacho, chagua kitu ambacho unaona ukivumilia kukifanya kitakupa mafanikio makubwa maishani mwako. Kisha jitoe kukifanya hicho kama ulivyopanga bila kuruhusu kisingizio chochote. Hakika litabaki suala la muda tu utafanikiwa.
Kufahamu zaidi kuhusu UVUMILIVU na NIDHAMU na jinsi vinavyoweza kukusaidia kujenga mafanikio unayoyataka, hakikisha unakipata kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Kitabu hiki kwa sasa kinauzwa kwa bei ya ofa ya sh. 15,000/ badala ya sh 20,000/. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kupata kitabu hiki leo kabla ya ofa haijaisha.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz