Jiunge Na Programu Hii Utoboe Mwaka Huu 2023, Vinginevyo……
[ ] Umeyafikisha wapi malengo uliyoyapanga Januari 2023?
[ ] Malengo mangapi ya mwaka 2023 bado unayakumbuka mpaka sasa?
[ ] Iko wapi hamasa ya kufanya makubwa uliyokuwa nayo Januari 2023?
[ ] Je hujaanza kuishi kwa mazoea uliyokuwa unaishi mwaka 2022 na kukufanya uumalize mwaka kwa unyonge?
[ ] Unafanya nini unapokutana na ugumu, je unakata tamaa?
Kama majibu ya maswali hayo machache yanakupa wasiwasi wa kuuishi mwaka 2023 kwa mafanikio, nakushauri ukimbilie kwenye programu ya JENGA NIDHAMU 2023.
Hii ni programu itakayokusaidia kujenga tabia ya NIDHAMU KALI. Hii ni tabia inayokuwezesha kufanya ulichokipanga bila kusikiliza sababu yoyote ile. Unafanya ulichopanga uwe unajisikia au hujisikii.
Kujenga tabia hii utachagua kitu kimoja ambacho utakifanya kila siku kwa mwaka mzima bila kuacha hata siku moja. Pale utakapokosa kukifanya kitu hicho kwa siku tatu mfululizo, utaondolewa kwenye programu hii.
Unachagua nini? Je …
- Kuamka mapema kila siku saa 11 kamili alfajiri au kabla na kuianza siku yako kwa ushindi?
- Kuweka akiba kiasi chochote kila siku kwa mwaka mzima na mwisho wa mwaka kuwa na mtaji wa kuanzishia biashara.
- Kumtafuta mteja mpya wa biashara yako kila siku na hivyo kuongeza kuikuza biashara yako?
- Kusoma kitabu kila siku bila kuacha hata siku moja na kufanikiwa kumaliza angalau kitabu kimoja kila mwezi?
- Kuandika kila siku na kufanikiwa kuandika kitabu ulichofikiri kwa miaka mingi sasa?
- Kufanya mazoezi kila siku na kuimarisha afya yako?
- Kuandika ndoto, malengo na mipango yako kila siku na kisha kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa wewe halisi?
- Kuandaa orodha asubuhi ya vitu unavyokwenda kuvifanyia kazi kisha jioni kujifanyia tathmini na kuboreka kila siku?
- Kunywa maji kila siku kwa kiwango kinachoendana na uzito wako na kuepukana na magonjwa mengi ambayo yangeweza kukupata?
- Kuweka na kuifuata bajeti kila siku kwa maandishi
Habari njema ni kuwa Programu hii ni bure kabisa. Hutatoa fedha yoyote zaidi ya kujitoa wewe mwenyewe.
MAHITAJI
- Simu janja yenye app ya telegram
- Chagua nidhamu moja kati hizo 10 hapo juu au nyingine ambayo utaweza kuifanya kila siku na kutoa ushahidi
- Utayari wako
HATUA ZA KUCHUKUA SASA
• Kama huna app ya telegram kwenye simu yako pakua sasa.
• Bonyeza kiunganishi hapo chini
https://t.me/+uftysBbpBl4zODE0
• Ukishajiunga na kundi hilo, jitambulishe, ainisha tabia unayochagua kuiishi na ushahidi utakaouweka.
Karibu sana.
Kwa swali lolote, wasiliana nami kupitia namba zilizopo hapa chini.
Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, Mwl & Mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz