Unaweza Kutotumia Zaidi Ya Kipato Chako.
Moja ya kitu kinachowakwamisha watu wengi kutengeneza utajiri na kufikia uhuru wa kifedha ni matumizi. Hizi ni fedha ambazo zikienda hazirudi tena. Mkwamo huo unakuja pale matumizi yanakuwa makubwa kuliko kipato.
[ ] Ukitumia zaidi ya kipato chako huwezi kupata fedha ya kuweka akiba.
[ ] Ukitumia zaidi ya kipato chako hutabaki na fedha ya kuwekeza.
[ ] Ukitumia fedha zaidi ya kipato chako itakulazimisha wewe kukopa. Hii huitwa mikopo mibaya kwani ni fedha ambazo ukizikopa hazizalishi.
[ ] Ukitumia zaidi ya kipato chako ni vigumu sana kukusanya fedha taslimu nyingi na kufikia utajiri
Kwa sababu mikopo mingi huwa na riba, hivyo itakulizimu kutoa fedha nyingi zaidi ya kile kiasi ulichokopa.
Imebainika kuwa kipato kinapoongezeka na matumizi pia huongezeka. Hivyo suala la kuweka akiba si kwa sababu ya kuwa na kipato kidogo bali nidhamu kali ya kutumia kipato chako kwa busara kubwa. MATUMIZI YAKO YASIZIDI KIPATO CHAKO
Ili kuweza kuweza kuongeza kipato chako na kufikia utajiri mkubwa huna budi kujenga nidhamu kali ya jinsi ya kutumia fedha zako. Mara zote usitumie zaidi ya kipato chako.
Ili kuweza kufanikiwa katika hilo huna budi kujenga nidhamu weka bajeti kweye kila kipato unachokipata. Weka vipaombele kwenye fedha ya matumizi.
Katika kuweka bajeti usisubiri mpaka upate fedha ndipo uanze kufikiria uzifanyie nini. Bali weka mpangilio mapema namna utakavyotumia fedha yoyote ile utakayoipata.
Unaweza kugawa fedha zao kwenye mafungu haya; Akiba(10%), dharura(10%), matumizi(60%), uwekezaji (10%), maendeleo binafsi (5) na misaada(5%).
Ukishakuwa na mafungu haya kabla ya kupata fedha inakuwa rahisi kujenga na kuiishi nidhamu ya matumizi ya fedha kuliko kusubiri upange namna ya kuigawa fedha hiyo baada ya kuipata.
Lakini pia baada ya kujua kiasi halisi cha fedha ya matumizi ambacho utakipata kutegemeana na kipato ndipo unapotakiwa kuweka bajeti ya fedha hiyo ya matumizi na kuhakikisha hutumii zaidi ya kisi hicho.
Hapa ndipo nidhamu inapotakiwa kufanya kazi. Hapa ndipo msukumo wa ndani wa kuzikataa baadhi ya tamaa unatakiwa. Hapa ndipo unapotakiwa kuikumbuka KWA NINI KUBWA ya kugawa na kuheshimu mafungu ya fedha.
Zifuatazo ni mbinu unazoweza kutumia kuepuka matumizi yako hasizidi kipato
- Gawa kipato chako katika mafungu kabla ya kuzipata fedha hizo( imezungumziwa vizuri hapo juu)
- Zipeleke fedha nyingine sehemu zinakohusika mara tu baada ya kupata kipato hicho huku ukibakiwa na fedha ya matumizi
- Weka baje ya matumizi huku ukizingatia vipaombele
- Epuka kununua kitu ambacho hakipo kwenye bajeti
- Usifanye mashindano ya kununua vitu na mtu yoyote
- Usikimbilie kukopa ili kufanya matumizi ya ziada bali jifungie kwenye bajeti yako
- Jifanyie tathmini kila siku namna unavyotumia fedha zako. Utagundua kuna sehemu ambayo unahitaji kukaza nidhamu ya matumizi yako.
Itakuwa ni vigumu kutengeneza utajiri kama hutafanikiwa matumizi yako yatazidi kipato. Ili jitihada za kukuza kipato chako ziweze kukufikiwa kwenye uhuru wa kifedha huna budi kuhakikisha kwanza matumizi yako hayazidi kipato chako. Kisha endelea kuongeza kipato na malengo ili kipato chako kiweze kuwa na mfungu mengine kama vile kuwekeza na kuanzisha biashara.
Haya yote yatawezekana kama utajenga nidhamu kali ya kuhakikisha unafanya kile ulichopanga kuhusu fedha zako.
Chukua hatua leo.
1.Kaa chini kisha tafakari namna unavyoweza kugawa kipato chako chochote utakachokipa(unaweza kutumia mfano hapo juu).
- Baada ya kujua ni kiasi gani cha kipato kinaenda kwenye matumizi, jitahidi kujenga tabia(nidhamu) ya kuhakikisha hutumii makundi mengine kwenye matumizi. Inaweza kuwa ngumu mwanzoni lakini baadaye itakuwa nia tabia yako.
Asante.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz