Anza Na Ukuaji Huu Kujihakikishia Mafanikio.
Mtoto akizaliwa na kuendelea kubaki na uzito uleule bila ya kuongezeka atashangaza sana. Jitihada mahususi zitachukuliwa ili kwanza kujua tatizo alilonalo na pili kulitatuta tatizo hilo.
Hiki ndicho kinachotakiwa kufanyika pia katika maisha ya mtu. Kama unaona muda unazidi kwenda lakini kuna hatua ndogo sana unazipiga au hakuna hatua kabisa huna budi kujiuliza tatizo ni nini na kitu gani unapaswa kufanya kubadili hali hiyo.
Matokeo mazuri ya mtoto huanza na mabadililo sahihi ndani yake. Kuongezeka kwa uzito wake hutegemea umeng’enywaji mzuri wa chakula ndani yake pia na kutokuwepo kwa maradhi ndani yake.
Vivo hivyo ili uweze kupata matokeo makubwa na mazuri nje yako ni lazima kuwe na ukiaji mzuri ndani yako. Changamoto nyingi unazokutana nazo zitatatuliwa kwa wewe kuanza kufanya mabadiliko ndani yako.
Natokaje hapa nilipo?
Nitaweza kweli kufanya hili jambo?
Nitaanzia wapi?
Nini nifanye?
Haya ni baadhi ya maswali ambayo wengi hujiuliza kutafuta sluu ya changamoto wanazokutana nazo. Katika hali kama hii changamoto huwa zinakuwa zimemtawala mtu kiasi cha kutojua nini akifanye au atokee wapi.
Hali hii hutatuliwa kwa mtu mwenyewe kuanza kukua kwanza ndani yake. Kukua ndani yako ni;
[ ] Kuruhusu kufahamu zaidi ya unavyofahamu sasa
[ ] Kuruhusu kubadili mtazamo wako wa sasa
[ ] Kuongeza kujiamini mwenyewe
[ ] Kuongeza hamasa
[ ] Kuchukua hatua au uwajibikaji
[ ] Kuwa tayari kuvumilia
Moja ya njia ya uhakika ya kufanikiwa kukua ndani yako ni kupata maarifa na kuwa tayari kuyatumia au kuyaishi.
Licha ya watu wengi kutokuweka kipaombele kikubwa kwenye usomaji wa vitabu, lakini fahamu kuwa kusoma vitabu kimekuwa kipaombele kwa kila mtu aliyepata au anayetafuta mafanikio makubwa.
Haya ni baadhi ya mambo makubwa yanayotokea pale unapoanza kusoma vitabu na kuyatumia maarifa hayo;
[ ] Kukubali mtazamo hasi kuwa chanya. Kumbuka mtazamo ndiyo mwanzo wa chochote unachofanya na kukipata.
[ ] Kupata maarifa mazuri ya watu waliombali na usioweza kuwafikia
[ ] Unapata maarifa ya watu waliofanya makubwa lakini walishafariki
[ ] Unapata sluu ya changamoto unazopitia. Changamoto unazopitia sasa kuna watu walishazipitia, wakazitatua na sluu zake wakaziandika kwenye vitabu
[ ] Utapata hamasa ya kufanya makubwa. Kama kwa wengine yaliwezekana, basi hata kwako pia
[ ] Kinakuwa kama kioo cha tabia zako.
Unaweza kutambua kama unaishi tabia za mafanikio au laa!
Pata picha hayo yote yametokea katika maisha yako, ni kwa kiasi gani utapiga hatua? Naamini utapiga hatua kubwa.
Utafanikiwa kuanza na kuishi kwenye kusoma vitabu kama utalipa jambo hili kipaombele. Kipaombele hicho kitafanikiwa kama utajenga nidhamu kali juu ya usomaji vitabu.
Hivi ndivyo unavyoweza kujenga nidhamu kali ya kusoma vitabu na kupata manufaa
[ ] Weka bajeti kwa ajili ya kununua vitabu. Uwekezaji waa kwanza lazima uwe ndani yako. Tenga fedha ya kununua angalau kitabu kimoja kila mwezi
[ ] Tenga muda wa kusoma kila siku. Anza hata kwa kusoma kurasa mbili kila siku
[ ] Andika pembeni mambo unayojifunza kila unaposoma
[ ] Unapomaliza kitabu, hakikisha una angalau jambo moja la kwenda kufanyia kazi katika maisha yako.
[ ] Jisukume kuchukua hatua hii muhimu ya kusoma. Kila wakati kumbuka mazuri unayoweza kuyapata kutoka kwenye kusoma vitabu.
Ndugu! Muda mzuri wa kupanda mti wa kivuli ilikuwa miaka ishirini iliyopita, lakini kama hukupanda muda mwingine ni sasa.
Chukua uamuzi wa kuanza kusoma vitabu leo bila kujali ni muda gani umeupoteza. Kwa kuanza chagua kitabu kimojawapo au vyote kwenye orodha hii:
1. AMSHA UWEZO WAKO HALISI. Hiki kitakuonyesha ngugu kubwa uliyonayo ambayo bado hujaitumia na namna ya kuiamusha ili uweze kupiga hatua kubwa zaidi. Umejipunja kwa siku nyingi, kataa sasa kuendelea kujidharau. Bei ya kitabu hiki ni sh. 10,000/
2. DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Kitabu hiki kinaweka bayana nguzo 12 za maisha ya mafanikio na namna ya kuzijenga. Nguzo hizo ni kama Uwezo na upekee, maono na melengo, nidhamu, …. uzuri wa kitabu ni kuwa unaweza kusoma dondoo moja tu kwa siku na kuchukua hatua. Unaweza kuisoma dondoo hiyo kwa dakika tano tu. Bei ya kitabu hiki ni sh 15,000/
- UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA. Unahangaika kupata wazo la biashara? Je unaona mtaji wako ni mdogo kuanzisha biashara? Ulikuwa na biashara lakini imekufa? Una biashara lakini inasuasua? Majibu ya maswali haya na mengine mengi yapo kwenye kitabu hiki. Bei ya kitabu hiki ni sh 15,000/
Kupata vitabu hivi wasiliana nasi: 0752 206 899.
Ungependa kuanza na kitabu kipi? Karibu upate kitabu na kuanza kutatua changamoto zako.
Asante,
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz