Usisimamishe Nguzo Kabla Ya kuchimba Shimo….Itaanguka Tu!
Kama utachukua nguzo na kuisimamisha juu ya ardhi bila kuichimbia shimo, tambua kabisa kuwa nguzo hiyo itaanguka tu. Hata kama utaamua kufanya kazi hiyo miaka elfu moja hutaweza kufanikiwa.
Ili nguzo isimamishwe inahitaji kuchimbiwa shimo kisha nguzo hiyo kutumbukizwa na kushindiliwa.
Umekuwa ukisimamisha nguzo maishani mwak, mpaka leo haijasimama na unajiuliza kwa nini? Nguzo za maisha yako ni jitihada unazoweka kila siku ili kupata mafanikio. Lakini shimo ambalo huchimbi ni mtazamo sahihi.
Tamaa ya mafaniko bila mtazamo sahihi ni bure.
Kuweka mipango bila mtazamo sahihi ni bure kabisa.
Kuwa na nguvu nyingi za mwili bila mtazamo sahihi ni bure.
Kuna jitinada nyingi umekuwa ukizichukua ili zikupatie matokeo ya mafanikio lakini zimeshindwa baada ya kukosa shimo la mtazamo sahihi ndiyo ungeweza kusimamia nguzo za mafanikio unazozihitaji.
Unaupenda utajiri lakini unaamini kuwa utajiri ni dhambi. Huwezi kuwa tajiri
Unatamani mafanikio makubwa lakini unajiona huwezi.
Unataka kupiga hatua lakini huamini kupata maarifa kama vitabu vya kukuza ndani.
Unataka kuwa mafanikio lakini unaamini kuna mtu wa kukuwezesha katika hilo. Sahau kuwa unayetaka.
Unataka kuwa na mafanikio maishani mwako lakini lakini hutaki kufanya kazi. Mafanikio utayasikia hewani.
Unataka kupendwa lakini wewe hupendi wengine. Hii ni ngumu unachokitoa ndicho ukipata.
Ili uweze kufikiri, kuamua na kufanya unachokitaka huna budi kuwa na mtazamo sahihi wa kushikilia kile unachotaka.
Mitazamo mitano ya kuanza kuichimba kama shimo ili kuweza kusikilia mafanikio yako;
1. Inawezekana. Amini kwa thati kabisa unaweza kupata chochote unachokitaka ukiwa tayari kulipa gharama zake.
2 . Uwajibikaji . Amini kuwa unawajibika kwa 100% kwa kile unachokitaka maishami mwako.
- Kujitoa. Amini hakuna kitu kizuri kinakuja kirahisi, vinginevyo kila mtu angekuwa nacho. Jikane kukipata
- Kazi. Amini kuwa hakuna mafaniko bila kazi. Kufanya kazi sio utumwa. Jenga urafiki na kazi.
- Kukua . Amini kuwa maarifa sahihi ndiyo yatakuja ukuaji wa ndani utakaosababisha ukuuji wa nje.
Mtazamo una nguvu kubwa sana tofauti na ulivyokuwa unafikiri. Ukifanikiwa kuuweka vizuri mtazamo hakuna kinachoweza kushindikana maishani mwako; utawaza sahihi, utaamua sahihi na kutenda sahihi.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo mzuri sana wa kubadili mtazamo wako kuhusu nguvu kubwa uliyonayo. Kupitia kitabu hiki utatambua na kuamini nguvu kubwa uliyonayo kisha kupata mafaniko makubwa unayostahili.
Licha thamani kubwa ya kitabu hiki, kwa sasa unakipata kwa bei ya promotion ya sh 10,000/. Usiendelee kujipunja kwa sababu ya mtazamo kipate kitabu na kuanza maisha yako halisi. Wasiliana; 0752 206 899.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz