Tai Aliyegeuka Kuwa Kuku .


Categories :

“Toka Uliko, Una hadhi Ya daraja La Kwanza”

Mwindaji mmoja akiwa porini alimuona tai akitoka kwenye kiota. Alipopanda kwenye mti uliokuwa na kiota hicho ndipo akalikuta yai moja, alilichukua na kwenda nalo nyumbani.

Alipofika nyumbani akalichanganya lile yai na mayai ya kuku ambaye ndiyo alikuwa anaanza kuatamia. Baada ya siku kadhaa kuku yule alitotoa na kifaranga mojawapo kikawa ni cha tai.

Kifaranga cha tai kiliendelea kujichanganya na vile vya kuku huku kikiona kama ni wenzake. Pia hata vifaranga vya kuku vilimuona tai kuwa mwenzao. Chochote kilichofanywa na vifanga vya kuku na kile cha tai kilifanya. Vifaranga vyote vilikua na kuwa ndege wakubwa huku na yule tai akiendelea kutembea tu ardhini.

Siku moja yule tai wa kufugwa alimuona tai pori akiwa anaelea angani kwa uhuru na kwa ufanisi mkubwa, ndipo alipowauliza wale kuku aliofikiri ni wenzake, yule ni nani, mbona ana uwezo mkubwa sana wa kuelea angani na sisi hatuwezi?

Ndipo wale kuku wakamuambia kuwa sisi ni kuku maisha yetu ni ya ardhini na hatuwezi kuelea kama yule tai. Tai yule aliridhika na lile jibu na akaendelea na maisha ya ardhini na ndugu zake mpaka siku ile yule mwindaji alipoamua kumchinja na kumla.

[ ] Mazingira yaliyokukuza yamekutengeneza wewe wa leo

[ ] Umeambiwa wewe ni wa kawaida, umekubalia

[ ] Umeambiwa huwezi kuwa na ndoto kubwa, umekubali

[ ] Umeambiwa huwezi kuwa tajiri, umekubali

[ ] Umeambiwa huwezi kuwa maarufu, umekubali

[ ] Umemabiwa huwezi kufanya makubwa ya kushangaza dunia, umekubali

Ndugu! Wewe ni wa thamani kubwa maradufu ya ulivyoambiwa na kuamini. Una uwezo mkubwa na wa pekee ndani yako lakini bado umelala kama ule uwezo wa tai wa kuruka.

Kuna kitu kimoja tu cha kukutoa huko ulipo na kuhamia daraja la kwanza. Nacho ni kubadili mtazamo na kuuona ukuu wako.

Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo unaoweza kugeuza kabisa mtazamo wako uliolaza usingizi mzito uwezo wako kisha kuuamsha na kukuwezesha kufanya mambo makubwa unayostahili. Kitabu hiki unakipata leo kwa bei ya punguzo, sh 10,000/. Wasiliana: 0752 206 899. Usizidi kuchelewa kuruka tena, pata kitabu na anza kuutumia vyema uwezo mkubwa uliolala tu ndani yako.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *