Usipasue Yai Kuangalia Ukuuaji wa kifaranga, Subiri Muda Wake; Kitatoka tu!


Categories :

Unafahamu kuwa ili kifaranga cha kuku kiweze kupatikana basi ni lazima yai liatimiwe ama kwa kuku mwenye au kwa kutumia mashine.

Kwa kulifahamu hilo umekuwa mwaminifu sana kusubiri kwa takribani siku 21 ili kukishuhudia kifaranga kikitoka.

Hakuna hata siku moja uliposema natamani kuona kifaranga kinaendeleaje hivyo ukavunja yai ili kuona ni kwa kiasi gani kifaranga kimekua.

Umekuwa hufanyi hilo kwa sababu unatambua kwa dhati kabisa kuwa ukilivunja yai hilo ndiyo utakuwa umekosa kabisa kifaranga kwa kuwa muda wake ulikuwa bado.

Kumbuka kitu ambacho kimekuwa kikikuwezesha kupata kifaranga ni uelewa, uvumilivu na nidhamu.

Lakini uelewa huo na uvumilivu huo hujahamishia kwenye ndoto, malengo na mipango yako!

Kwa nini kila siku unawaza kufanya kitu tofauti? Umeona kuna biashara fulani unaweza kuifanya, umeweka mipango, lakini umekuwa unasikia kuna nyingine zainalipa zaidi unabadili wazo la awali. Ndiyo maana mpaka hujaanza biashara yoyote.

Umefanikiwa kuanzisha biashara, lakini umekosa uelewa, umamini kuwa inatakiwa ikupe mafanikio haraka, umepasua yai kwa kuisusa.
Komaa nayo, inakua kidogo kidogo na itakulipa tu.

Umepanga kuwa utakuwa unaweka akiba kutoka kwenye vipato vyako ili kuja kufanya fulani maalumu. Ulijiambia kuwa hutaigusa kamwe. Kwa nini umengia tamaa, umeichukua na kifanyia matumizi mengine nje ya ule mpango wako? Imelipasua yai kuangalia ukuaji wa kifaranga.

Umewekeza fedha zako kwenye maeneo tofauti tofauti. Ulisema hizi ni kwa ajili ya kuendelea kukua kukupa utajiri hapo baadaye. Kwa nini sasa unataka kuzitumia kwa sababu hazikui haraka. Unatambua kuwa faida ya uwekezaji hupatika baada ya fedha ya kukaa kwa muda mrefu. Huku ni kupasua yai ili kuangalia kifaranga kinaendeleaje.

Ndugu umekuwa hupati matokeo kwa sababu kila unachokianzisha hakifiki mwisho. Unakata tamaa kwa matokeo kucheleaa. Endelea kuatamia jitihada zako.

Lazima ujenge nidhamu kali ya kuhakikisha ulichopanga kufanya bila kujali vishawishi vinavyokuzunguka.

Unatakiwa kujenga nidhamu ili uendelee kuweka jitihada hata pale matokeo yanapochelewa.

Jenga nidhamu ya kuhakikisha unayatengenezea malengo yako mazingira mazuri kwa ajili ya kukupa matokeo. Kumbuka kuku huyaatamia mayai ili kuyapa joto na unyevuu kiranga kikiue!

Baada ya kujenga ndoto yako kamili na kuweka malengo mizuri basi endelea kuyaatamia kwa kuweka hatua sahihi:

[ ] Yaandike malengo yako kila siku

[ ] Yafikiri malengo yako kila wakati

[ ] Yaani malengo yako

[ ] Jifunze kuhusu malengo yako kila siku

[ ] Shirikiana na wengine kuhusu malengo yako

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *