Umeuongeza Uzito Mwenyewe.


Categories :


“Usishikilie Kinachokuumiza Kwa Muda Mrefu”
 
Watu wengine walijifunza na kutua mizigo yao na wewe lisome somo hili kwa umakini mkubwa. Hakika hutateswa na mizigo hiyo kamwe.
 
Akiwa kwenye mafunzo ya kukabiliana na maisha ya dunia hii iliyojaa kila aina ya changamoto na makwazo mengi dada mmoja alikuja na glasi ikiwa imejaa maji na kuwa uliza wahudhuriaji kukadiria uzito wa glasi ile yenye maji ndani yake na kama ingekuwa nzito kuibeba au la!
 
Wapo waliosema gramu 300 wengine 400 na wengine 500. Lakini wote walisema itakuwa ni yepesi tu kuibeba. Aliwaambia wote wamepata kwa kufikiri tu ni uzito gani ile glasi ingekuwanao kama ingekuwa imewekwa kwenye mzani.
 
Dada yule akaendelea kusema uzito wa ile glasi kwa yeye aliyeishikilia utatofautiana kutokana na muda atakaoushikilia. Kama ataishikilia kwa dakika moja tu kisha kuiweka chini, hakutakuwa na tatizo na glasi hiyo itaonekana ni nyepesi sana.
 
Lakini kama akiendelea kuishikilia kwa saa moja nitaanza kuiona glasi hii kuwa nzito sana na nitatamani niiweke chini. Lakini kama nikiendelea kuishikilia kwa muda mrefu, zaidi ya masaa mawili, hali ya mkono wangu itakuwa mbaya na misuli ya mkono itakakamaa na kusababisha maumivu makali ya mkoni na hata kuidondosha glasi hiyo na kuipasua.
 
Lakini kumbuka kuwa glasia ya maji ni ile ile na na ujazo ni ule ule. Kitakachokuwa kinaniumiza sio kuongezwa kwa uzito wa glasi bali muda nilioshikilia glasi hiyo.
 
Dada Yule alisema jaribio hilo ni uhalisia unaoendelea katika maisha ya watu. Dunia imejaa changamoto nyingi na zenye maumivu makali, zina uwezo wa kuumiza mioyo sana. Kupitia maumivu hayo ambayo watu wengi wanayapata yamekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwao kupiga hatua.
 
Lakini uzito wa changamoto hizo umeongezeka baada ya watu kuamua kuzishikilia kwa muda mrefu. Aliendelea kusema kuwa;
·       Mtu amepata changamoto ya hasara kwenye biashara yake, badala ya kukaa chini na kujiuliza nini cha kujifunza ili asipate changamoto tena, lakini yeye huendelea kuhuzunika na kuumia moyoni kwa muda mrefu kitu kinachomsababishia kufikiria kukata tamaa.
·       Mtu akikwazwa na mtu mwingine, baada ya kumpuuzia na kuendelea na safari yake yeye huanza kumfikiria kiundani na kujiuliza maswali mengi ndani yake ya kuwa mtu huyo amemuonaje?
·       Mtu akikosewa na mtu hata kama mkosaji huyo atakuja kuomba msamaha, yeye atakataa kutoa msamaha huo na hivyo kuendelea kumbeba mt huyo maishani mwake huku akiendelea kumuumiza.
·       Kuna magumu mtu anayapitia, mambo hayaendi badala ya kuamini kuwa ana uwezo ndani yake wa kubadili matokeo hivyo zidi kuweka nguvu kwenye malengo yeye huanza kulalamika huku akiamini kuna mtu amemsbabisha yeye awe kama alivyo.
 
Ndugu hili ni soma muhimu sana kwako. Umepata shida sana pale unapokutana na changamoto si kwa sababu ya ukubwa wa changamoto, bali muda ule ulioendelea kukaa nayo tena kwa mtazamo hasi.
 
Jambo hili limekufanya ukwame katika kupiga hatua za malengo yako. Baada ya kukusanya nguvu za kujifunza na kuchukua hatua kwa kile kilichotokea wewe umpoteza nguvu kwenye kushikilia jambo hilo kwa maumivu tena makali.
Badala ya kuachia maumivu hayo na akili yako kuweka umakini kwenye kuboresha, akili yako imeendelea kushikilia maumivu.
Badala ya kuboresha mahusiano na mtu aliyekukwanza na kuzidi kushirikiana, wewe ndiyo umezidi kumchukia na kumtenga mbali sana.
Badala ya kuja na mbinu za kufanya biashara yako kwa ufanisi zaidi na kupata faida , wewe bado umeishikilia maumivu yale ya kupata hasara.
 
Chukua hatua
1.     Kaa chini kisha tafakari ni maumivu gani uliyoyashikilia kwa muda mrefu sasa  huku yakiendlea kukuumiza kiasi cha kushindwa kuendelea kupiga hatua? Achilia leo, jifunze kisha songa mbele.
2.     Kuanzia sasa, ukipata changamoto yoyote, angalia cha kujifunza kutoa kwenye changamoto hiyo, tumia funzo hilo kuwa bora kuliko awali.  Itakuwa ngumu mwanzoni lakini ukiendelea kujisukuma, itakuwa ni tabia yako.
 
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *