Kuna Maumivu Aina Mbili Mbele Yako; Chagua Moja Kwa Busara.


Categories :

Maisha ni kuchagua. Hakuna kitu ambacho huwa kinatokea kwa bahati mbaya, vingi huwa ni machaguo yako. Maisha uliyonayo sasa ni machagua yako ya siku za nyuma.

Hata maumivu yana machaguo. Kuna machaguo makuu mawili ya maumivu, hayo ndiyo huleta mustakabali wa maisha yako. Busara yako ndiyo itaamua mwisho mwema au mbaya. Machaguo hayo mawili ni maumivu ya nidhamu au ya majuto.

Bahati mbaya au nzuri juu ya maumivu hayo ni kuwa huwezi kuyakwepa yote. Mwisho wa safari laizma uangukie kwenye maumivu mojawapo. Ila una nafasi kuchagua.

NIDHAMU ni kufanya kile unachokitaka kukifanya bila kuruhusu sababu yoyote ile ikuzuie. Huku ni kufanya hata pale unapokuwa hujisikii. Kumbe nidhamu ni kujilazimisha kufanya kujilazimisha huleta maumivu ndiyo maana watu wengi hukwepa.

Maumivu haya hutangulia matokeo.
Matokeo ya nidhamu ni kupata kile unachostahili tena huwa kikubwa. Watu wanaochagua kuvumilia ni wale u unaowaona wana mafanikio makubwa leo. Kama ni utajiri basi tambua kuwa matajiri hao walichagua maumivu ya nidhamu.

Miongoni mwa maumivu yanayotokana na nidhamu ni;

[ ] Kuuacha usingizi mtamu asubuhi kisha kuamka na kuianza siku mapema

[ ] Kujizuia kutumia akiba waliyoweka hata kama kuna vitu vizuri wanavitamani sana.

[ ] Kuwaacha baadhi ya watu uliozoeana nao

[ ] Kuacha kufuatilia mambo uliyoyazoea ambayo hayana mchango mkubwa kwako kama kushabikia michezo na siasa

[ ] Kuendelea kuulazimisha mwili wakokufanya kazi pale unapokuwa unajisikia kuchoka.

Katika maumivu hayo ndipo unapohitaji nidhamu kali ya kukuwezwsha kuyakabili maumivu hayo na kupata matokeo adimu. Watu wachache sana huwa tayari kuyakabili maumivu huku wengi wakitafuta sababu za kutochukua hatua.

MAJUTO. Majuto ni mjukuu washahili husema. Hii ina maana kuwa majuto ni maumivu ambayo huja baada ya kutokufanya kitu fulani. Kitu hicho ni kutokubali maumivu ya nidhamu.

Maumivu haya huwa ni makali sana kwa sababu ya;

[ ] Ya kutokuwa na nafasi tena ya kushanya kile ulichokwepa licha ya kuwa na utayari sasa

[ ] Kuongezeka kwa tatizo dogo ulilokuwa nalo.

[ ] Kutokuwa na muda tena wa kufanya kitu hicho, hasa pale unapoambiwa unakaribia sana kufa.

Upo hapa duniani kutoa matokeo. Matokeo hayo yana thamani sana kwa watu. Matokeo hayo ni yanatatua changamoto za watu.

Lakini thamani unayoweza kuitoa, haiji bure bali kwa nidhamu kali ya maumivu. Lakini ili uweze kuishi kikamilifu hapa duniani huna budi kutoyakimbia maumivu ya nidhamu. Ulinde muda wako ulionao kwa kujitoa kuishi nidhamu na kupata matokeo makubwa unayostahili.

[ ] Chagua kitu kimoja au vichache ambavyo moyo wako unakushuhudia kuvifanya

[ ] Ainisha gharama(maumivu) unazotakiwa kuzilipa

[ ] Weka malengo ya kuanza kuzilipa gharama hizo

[ ] Vumilia maumivu hayo mpaka uyapate matokeo

Kuna maumivu mawili mbele yako usichague majuto, haya ni makali sana. Chagua kuishi nidhamu ili uweze kuishi maisha yako halisi.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *