Kamwe Usishindwe Kabla Hujafanya.


Categories :

Kuna matokeo ya utofauti ambayo ungekuwa umeyapata tofauti na uliyonayo sasa kama ungekuwa umefanya.

[ ] Naogopa kuanzisha biashara kwa sababu naweza kukosa soko

[ ] Nasita kuanzisha biashara kwa sababu naweza kupata hasara

[ ] Siwezi kwenda kumuomba msaada mtu huyo kwa sababu nafikiri atanikatalia

[ ] Naona kama hakuna maana ya kuweka akiba kwa sababu naweza nisiishi muda mrefu.

[ ] Hii ni fursa kubwa mno, sitaweza.

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo watu wengi wamekuwa wakizisema pale wanapofikiria kufanya kitu. Lakini pia ni kauli ambazo zimewazuia wengi kutochukua hatua.

Matokeo hasi tarajiwa yamekuwa kikwazo kwa watu wengi kutochukua hatua. Matokeo ambayo hayaonekani yamesimama mbele na kuzuia wasichukue hatua.

Mtazamo hasi wa matokeo ambayo unaweza kuyapata kabla hujaanzisha kitu imewafanya watu wengi kutoanzisha vitu. Fikria ni mara ngapi sasa umeahirisha kuanzisha biashara kwa sababu tu unaona utakosa wateja au utapata hasara?

Ni mara ngapi umekosa fursa kubwa kutoka kwa mtu kwa sababu tu ya kuogopa kuwa utakujibu hapana?

Ni mara ngapi umeamua kufanya vitu vya kawaida kea kuogopa kuwa huna uwezo wa kufanya mambo makubwa?

Kuna laana huwa inasimama kati ya mafanikio na mipango yako. Laana hiyo ni kuanza. Kujilazimisha kuanza kitu ni kutoa laana ya kukosa mafanikio.

Kutokuanza ni laana kwa sababu hakuna matokeo yoyote mpaka pale utakapoanza kufanya.

Pia ni laana kwa sababu hakuna uboreshaji wowote unaoweza kufanya kama hujaanza. Anza pata matokeo ndipo boresha. Usiishie kuhofia kuanza kwa sababu ya nafasi ya kupata matokeo hasi.

Ndugu mafanikio uliyoyasubiri muda mrefu yapo kwenye kuanza mipango ya malengo yako uliyoyaahirisha kwa muda mrefu kwa kuogopa kushindwa.

Usikubali kushindwa kabla hujafanya kitu hicho. Kaa chini na tafakari kitu ambacho umekuwa ulikiahirisha kukianza kwa kuhofia kupata matokeo hasi. Anza kufanya kitu hicho. Usiogope kwani matokeo hayo hasi yanaweza yasitokee. Au kama yakitokea yanaweza yasiwe kwa ukubwa unaodhania. Lakini pia kuna nafasi ya kuboresha.

Nini unakataa kushindwa leo hata kabla hujaanza?

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *