Ulizaliwa Kama Muujiza, Umepotezea Wapi Ukuu Huo?
Ulizaliwali na kupewa majina mazuri ya kila aina. Wapo waliokuita malaika, wapo waliokuita muujiza, wapo waliokuita shujaa, wapo wliokuona kama Rais. Umepotezea wapi umaarufu huo?
Ulipokuwa mototo watu walikuuliza unataka kuwa nani ukiwa mkubwa? Wewe uliwajibu kwa uhakika kabisa kulingana na kile ulichokuwa unakisikia ndani yako. Nataka kuwa rubani, nataka kuwa daktari bingwa, nataka kuwa Kiongozi mkubwa, nakata kuwa mnenaji maarufu, nataka kuwa tajiri. Je unachokifanya sasa ndicho ulichokisema kipindi hicho?
Ulipokuwa unakua ulijaribu vitu vingi sana bila ya woga. Hata pale uliapoanguka kwa sabbu ya kujaribu kusimama, lakini uliendelea mpaka pale ulipoweza kusimama na kukimbia. Mbona siku hizi unakuwa mwoga kujaribu vitu vipya vya kukupa matokeo mapya?
Kuna kipindi uliamini hakuna kinachoshindikana duniani. Ndiyo maana ulikuwa unang’ang’ani vitu kwa mzazi wako kiasi cha yeye kuamua kukopa fedha ili akununulie kwa sababu ya ung’ang’anizi usiokoma ulikuwa nao. Kwa nini siku hizi unakata tamaa haraka sana?
Umaarufu ulikokuwa nao utotoni ulikuwa unakuonyesha ukweli au uorijino wako. Hii ilikiwa ni ishara ya nani unatakiwa uwe baada ya kukua. Hii ilikuwa ni njia ya wewe kuifuata na kuishi kikamilifu hapa duniani.
Majibu uliyokuwa unayatoa kuwa unatarajia kuwa mtu fulani yalikuwa ni kweli kwani yalikuwa yanatoka ndani mwako. Sasa umebadili majibu yale na kuanza kuwa watu wengine tofauti na wewe uliokuwa unasema kipindi cha utoto wako. Umefanya hicho kwa kuwaiga watu wengine wanafanya nini badala ya kujiuliza wewe unaweza kufanya nini.
Umaarufu ule umepotea na sasa umekuwa mtu wa kawaida. Hii ni kwa sababu umeisikiliza maoni ya dunia ya kuwa wewe ni nani.
· Watu wamekuambia huna uwezo na huwezi kufanya makubwa, umekubali ndiyo maana unapanga malengo madogo tu kila siku ukiyaogopa makubwa.
· Watu wamekuambia wewe huwezi kuwa maarufu tena, umekubali na umewafuata wao.
· Umepanga kufanya jambo na ulipopata majibu ya tofauti, umekata tamaa. Hii inaonyesha umeshapoteza ung’ang’anizi wa utototni mwako!
Umeua uorijino wako na uhahitaji kufufuka. Kama bado upo hai leo unaweza kufufua uorijino wako. Unaweza kuishi uhalisia wako. Unaweza kuonyesha umaarufu wako. Unaweza kufanya makubwa ya kushangaza.
Kaa chini kisha fikiri ni vitu gani ulivipenda kuvifanya sana utotoni na bado vinaongea ndani yako. Weka malengo na mipango ya kuanza kuvifanya hivyo. Hivi ni vitu vinavyogusa ndoto ya maisha yako. Endelea kuboresha mawazo hayo kuwa kitu kikubwa na kilicho
wazi.
Kwa kufanya kitu hicho ndipo utafanikiwa kuamsha nguvu yako ya pekee na kuweza kufanya mambo makubwa. Umejipunja kwa sababu ya kuacha uorijino wako na kuamua kuishi maisha mengine. Urudie uorijino wako uubebe umaarufu wa utotoni ukubwani.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwanasayansi, mwl & mwandishi(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz