Ona Ulivyoshiriki Kumuua Huyu Babu!
Kuna tajiri mmoja alitoka nje ya nyumba yake nyakati za usiku na kumkuta babu akiwa amekaa nje ya nyumba yake. Kwa sababu ya baridi kali ya siku hiyo babu huyo alikuwa amejikunyata huku akitetemeka.
Ndipo yule tajiri akamuuliza kwa nini alikuwa hajavaa koti zito au kujifunika blankenti zito ili kujikinga na baridi? Yule babu akajibu kuwa licha ya kukosa sehemu ya kulala lakini ana koti ambalo amekuwa akijifunika wakati wa usiku. Lakini muda huo hakuwa nalo kwani alilisahahu sehemu aliyokuwa amekaa mchana.
Yule tajiri akamwambia usiwe na wasiwasi, ngoja niingie ndani nikuletee koti ujifunike na kujikinga na baridi.
Yule tajiri alipoingia ndani hakwenda moja kwa moja kuchukua koti badala yake akajisemea moyoni ngoja aangalie kitu sebuleni na kisha uataenda kumchukulia baada ya hapo. Alipofika sebuleni akakuta kuna taarifa ya kusisimua kwenye runinga ndipo akaa ilia aiangalie vizuri.
Baada ya muda kupita na ile taarifa kuisha akaingia chumbani kwake na kulala. Usiku wa manane ulipofika na kuzinduka usingizini ndipo akakumbuka kuwa kuna babu yupo nje na alimuahidi kuwa anaenda kumchukulia koti.
Tajiri yule akachukua koti mara moja na kutoka nje haraka ili kuweza kumsaidia yule babu. Alipofika nje akamkuta yule babu akiwa amefariki. Lakini babu yule alikuwa ameshika kikaratasi mkononi kikiwa kimeandikwa “Usingeniahidi ningeenda kufuata koti langu kabla nguvu hazijaniishia lakini nimeendelea kukusubiri uniletee koti bila mafanikio, ona sasa nakufa!”
Baada ya kusoma ujumbe ule yule tajiri alishikwa na uchungu mkubwa sana na kujilaumu kwa nini hakwenda moja kwa moja kuchukua koti muda ule!
Umeua vingi. Kuna sehemu ya kubwa ya maisha yako imekufa kwa sababu uliahidi lakini hukutimiza.
Umeweka mipango mingi na mizuri na ya kukuvusha lakini hujachukua, imekufa.
Gusa mara moja. Hii ni njia pekee ya kuwa na ufanisi mkubwa kazini na kupata matokeo maishani mwako. Ukishaamua kufanya kitu anza kukifanya hapohapo mpaka umalize bila ya kwenda kuanza kingine.
Ndugu sababu mojawapo ya kukosa matokeo kwenye maisha yako ni kusema nitafanya baadaye. Nitafanya baadaye imekuwa chanzo kikubwa cha kuahirisha na hivyo maisha yako kubaki palepale. Anza sasa kuishi nidhamu hii muhimu ya kufanya ulichopanga mara moja, utaona mabadiliko makubwa chanya utakayoanza kuyapata.
Ili kukujengea nidhamu kali ya kupata matokeo, AMSHA UWEZO ina programu ya kukusaidia wewe kujenga nidhamu. Kwenye programu hii unachagua jambo moja ambalo utalifanya kila siku bila kuacha kwa siku zilizobaki za mwaka. Je utachagua kuweka akiba kila siku, kuamka mapema kila siku, kusoma, kuandika kila siku, kufanya mazoezi kila siku,…? Kwa sababu utakutana na watu wengine wanaojenga nidhamu kama wewe itakuwa rahisi kwako kuhamasika kisha kujisukuma.
Programu hii ni buree kabisa. Hakikisha simu yako ina app ya telegram kisha bonyeza kiunganishi hicho. Gusa mara moja hapa https://t.me/+uftysBbpBl4zODE0
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz