Huwezi Kukua Zaidi Ya Hapo Mpaka Umefanya Hiki.
Kukua na kufikia mafanikio makubwa limekuwa tamanaio la watu wengi. Lakini wapo waliosubiri ngazi ya mafanikio hayo kwa muda mrefu sasa bila mafanikio.
Lakini wapo pia walioondoka hapa duniani yaani kufa bila ya kufikia ngazi waliyotamani au waliyostahili
[ ] Kuna kiasi fulani cha kipato ungetamani uwe nacho ili kikupe uhuru wa kifedha.
[ ] Kuna kiasi fulani cha ubora wa mahusiano ungetamani uwe nacho lakini bado upo mbali sana kukifikia.
[ ] Kuna aina fulani ya mtu unatamani ungekuwa nayo ambayo ungeona umekuwa wewe halisi
[ ] Kuna jambo fulani unaona ungelifanya ndipo ungepata ridhiko la moyo.
Inawezekana umejaribu mara kadhaa kufikia hatua hiyo lakini hujafika mbali, kisha umerudi kwenye ngazi ileile ya chini. Unajiuliza kwa nini?
Hapa kuna kitu huwa kinakosekana. Huwa unaanza ukuaji wa nje kabla ya ndani.
Ndugu, ukuaji wowote wenye mafanikio huanzia ndani. Yaani akili yako lazima iwe na picha kamili ya nini unachotaka kupata hata kabla ya jitihada za nje.
Baada ya picha kamili, ili picha hiyo iweze kuzaa matunda, inahitaji kiungo kingine kutoka ndani yako tena, kiungo hiki ni imani.
Ukishajua nini unataka lazima pia uamini kuwa hiyo picha unayoiona itaenda kutokea.
Bila kuwa na picha kamili ya nini unataka na imani kuwa unachokitaka tayari ni chako, ni vigumu kujisukuma kufikia ukuaji wako halisi.
Kusema natamani kuwa na kipato cha kutosha haitoshi. Unahitaji kujenga picha ya kiasi gani cha fedha unakihitaji ili kikupatie uhuru huo.
Kujua kiasi unachokitaka pekeyake haitoshi mpaka pale utakapokuwa umeamini kuwa kiasi hicho utakipata na ni cha kwako.
Changamoto ya kukua na kufikia ngazi tunayotaka huanzi hapa kwanza kwenye imani ya kuwa kiasi kikubwa cha mafanikio unachohitaji ni kujua kiasi hicho lakini akili yako kukupinga vikali kile.
Ni mpaka ushinde vita yako mwenyewe kwanza ndani yako hata ndipo utaweza pia kuweka nguvu za ziada nje yake.
Ishinde changamoto hii kwa kuamini kuwa una uwezo mkubwa ndani yako ambao bado hujautumia na hivyo unaweza kuuamsha ukapata mtaokeo ya kile unachokipenda.
Baada ya kushinda vita ya ndani kwako kinachofuata ni kuweka nidhamu. Hii ni vita nyingine ya kutokufanya kile ulichokipanga.
Utapata matokeo kama utajisukuma kufanya ulichokipanga hata pale utakapokuwa hujisikii. Kuweza kujisukuma zaidi huna budi kila wakati kujikumbusha matokeo mazuri unayotarajia kuyapata.
Ukuuaji gani unataka kuufanya maishani mwako?
[ ] Anza kwa kujenga picha kamili na ya wazi juu ya kitu hicho.
[ ] Pili amini kuwa ndani yako una uwezo mkubwa wa kukuwezesha kupata unachokitaka.
[ ] Tatu weka mipango na nidhamu ya kuhakikisha unajisukuma na kupata kile unachokikiamini kisha kukua zaidi.
Anza kukua ndani kisha malizia nje.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz