*Hivi Ndivyo Ulivyojihakikishia Kutopata Mafanikio Bila Ya Wewe Kujua!*
Kwenye kupata mafanikio, kila mtu ana nafasi sawa. Hakuna mtu aliyependelewa. Lakini licha ya kuwa na nafasi sawa, bado kuna watu wanopata mafanikio wakati wengine wakishindwa.
Kama bado upo hai una nafasi ya kupata kile unachokitaka kwani unaweza kuweka malengo, mipango na nidhamu kisha kupata kile unachotaka.
Lakini kuna kitu kimoja kinachokupa uhakika wa kushindwa. Kama umekuwa unafanya kitu hicho bila kujua basi leo fahamu hiki. Kitu hicho ni KUKATA TAMAA.
Hakuna mafanikio mkubwa yanayopatikan kwa urahisi. Kuna kazi tena kazi kubwa ya kuweka ili upate mafanikio yako. Pia njia ya kuyaendea mafanikio ina kila aina ya vikwazo. Hii inapelekea watu wengi kukata tamaa.
Kukata tamaa ni kusimaaa na kuacha kuendelea na safari. Hakuna namna yoyote ile utafanikiwa kufika unakotakiwa kwenda kama utaacha kusonga mbele.
Lakini kwa upande mwingine kuna kitu kimoja kinachoweza kukupa nafasi ya kupata kile unachokitaka, nacho ni kuendelea. Unapoendelea kufanya ulichopanga licha ya magumu unayopata una nafasi ya kukipata.
Ni uvumilivu ndiyo unaovunja ukinzani. Mgunduzi wa taa za umeme Thomas Edison alifanya majaribio takribani elfu moja mpaka kufanikiwa. Hivyo unaweza kufikiri ni mara ngapi hakupata majibu aliyoyataka. Je angekakata tamaa leo tungekuwa na taa hizi?
Kwa nini wewe umeacha kufanya ambacho uliaamini kabisa matokeo yake yangekupa mafanikio makubwa? Kuacha huko ni kujihakikishia kuwa hutayapata tena. Lakini una nafasi ya kupata hicho tena licha ya kuwa ulishakata tamaa.
Kifufue kwa kuanza tena. Anzia ulipoishia na anza kwa ubora kuliko mwanzo. Kamwe usifikirie tena kuacha.
1.Je ulifunga biashara kwa sababu ya kuwa na mauzo hafifu. Ianze biashara tena lakini sasa anza kuwafuata wateja waliko usisubiri waje wenyewe
2. Je uliacha kazi baada ya kuona unalipwa kidogo? Rudi tena ila sasa fanya kazi kwa bidii na ubora zaidi kuongeza thamani; utalipwa zaidi.
Kila la kheri.
Kwa huduma za ushauri, vitabu, mafunzo na semina usisite kuwasiliana na mimi kupitia 0752 206 899.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz