Ugunduzi Wa Kwanza Kabisa Hapa Duniani Wa Kubadili Maisha Yako.


Categories :

Kuna gunduzi nyingi sana zimetokea hapa duniani kabla na hata baada ya kuzaliwa. Kuna ugunduzi kama wa ndege, meli, taa za umeme, kompyuta nk

Gunduzi hizo hapo juu zinaweza zisiwe na athari za moja kwa moja kwako. Lakini kuna ugunduzi mmoja ambao una athari ya moja kwa moja kwako. Ukiufahamu na kuuishi lazima maisha yako yabadilike.

Ugunduzi huo ni wa William James na aliuweka kwenye nukuu hii “The greatest discovery of my generation is that a human being can alter his life by altering his attitude” ikiwa na tafsiri kuwa ugunduzi mkubwa wa kizazi ni kuwa binadamu anaweza kubadili maisha yake kwa kubadili mtazamo wake.

Naamini kuna mambo unataka kuyapata maishani mwako. Lakini yapo mengine unayafanya lakini hupati matokeo unayotarajia. Kuna kitu kimoja ambacho unaweza kukifanya na kikabadili kila kitu nacho ni kubadili mtazamo.

Mtazamo ni namna unavyoviona vitu kisha kukulazimisha kuchukua uamuzi. Kwa mfano mtazamo wako ukoje juu ya kukosa au kuchelewa kupata matokeo? Kama unataka matokeo ya haraka tu hutaweza kuvumilia hatua ambazo zinachukua muda mrefu kukupa matokeo.

Je unachukuliaje suala la mafaniko yako? Kama unaona kuwa kuna mtu anawajibika kukupa mafanikio, basi kila siku utakuwa unawalalamikia. Lakini utayapata mafanikio yako baada ya kugeuza mtazamo wako kwa kuona kuwa unawajibika kwa 100% juu ya maisha yako.

Unauonaje utajiri, je ni mzuri? Kama unauona utajiri ni mbaya hutaupata utajiri huo mpaka pale utakapouona utajiri ni mzuri.

Je unaona unaweza kuwa tajiri? Kama unajiona huwezi kuwa tajiri ndivyo itakavyokuwa. Kutoka kwenye gereza hilo lazima ujione una uwezo wa kuwa tajiri, ndipo utakapojisukuma kuweka jitihada na kuupata.

Ndugu! Unaweza kubadili hali yoyote uliyonayo sasa kwa kubadili mtazamo wako wa sasa. Ona upande mwingine. Fikiri kinyume na sasa. Huu utakuwa mwanzo mzuri wa kupata matokeo ya utofauti.

Mabadiliko ya kweli yanaanza kwa kubadilika ndani. Tumia ugunduzi huu kubadili mtazamo wako kubadili mtazamo wa mambo ambayo hayakupatii matokeo unayotaka.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *