Haya Ni Mambo Sita Ya Kukomaza Akili Yako .


Categories :

Akili ni mwanzo wa mafanikio yako. Ili uweze kukuza mafanikio yako huna budi kuanza kwa kukuza akili yako kwani huko ndiko mawazo yenye thamani kubwa yanakotokea.

Zifuatazo nia njia unazoweza kutumia ili kukuza akilia yako;

  1. Songa mbele.
    Usipoteze muda ukijilaumu kwa kile ambacho huna au ulichoshindwa.

Kuna jinsi upo na unahisi umeshindwa kwa sababu kuna vitu huna. Usikae sana kujilaumu na kujidharau. Una uimara mwingine unao unaoweza kutumia huo kufanya makubwa zaidi.

Badala ya kujilaumu kwa kile ambacho huna, jikite kujivunia na kutumia uimara ulionao.

  1. Usizikimbie changamoto. Mafanikio ni kuzikabili changamoto. Ukikutatana na changamoto, tambua kuwa hivyo ni vihunzi kuelekea kwenye mafanikio. Hivyo ukikutana na changamoto tambua unahitaji kuzikabili ili upate kile unachokitaka.
  2. Chukua hatari.
    Ukitaka kufanya kitu kipya unakuwa huna uhakika wa matokeo, lakini kuna fursa kubwa pia ya kupata matoke o mapya na makubwa pale unapofanya vitu vipya.

Ili uweze kupata matokeo tofauti na yale uliyoyazoea kupata, huna budi kuchukua hatari na kufanya vitu vipya.

  1. Kuwa na furaha muda wote. Katika maisha utakutana na vitu ambavyo una uthibiti navyo kama vike kuweka malengo na kazi. Lakini vipo vitu ambavyo vinaweza kutokea na huna uthibiti navyo.
    Kwa mfano ni vigumu kuilazimisha mvua inyeshe au jua liwake.

Ili uwe na furaha maishani mwako, basi wewe shughulika na vile ulivyo na uthibiti navyo. Usihangaike na vitu usivyoweza kuthibiti.

  1. Jifunze kutoka kwa waliobobea. Wapo watu wanaovifahamu kiundani sana maarifa au ujuzi unaouhitaji. Jifunze kutoka kwa hao. Hawa watakufundisha kutokana na uzoefu wao.
  2. Jifunze kila siku. Kwa sababu mafanikio yanaanzia ndani yaani akilini, basi ni vigumu sana kutenganisha kujifunza kwa kusoma na mafanikio.

Kwa kusoma vitabu unapata chakula na kuipa akili yako afya njema. Unaposoma vitabu unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa watu wa mbali, kujifunza kutokana na makosa na mafanikio yao.

Haya ni mambo sita ya kuzingatia ili kuweza kukomaza akili yako. Kumbuka kukomaza akili yako ni kukomaza mafanikio yako.

Jipatie vitabu hivi leo ili kuanza kukoamaza akili yako mara moja.

  1. AMSHA UWEZO WAKO HALISI
  2. DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO
  3. UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA

Wasiliana: 0752 206 899 au bonyeza hapa https://wa.me/message/Q6IVWM4M5LFTG1

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *