Kinachoharibu Chuma Ndicho Kinachokuharibu Wewe…Usikubali


Categories :

Chuma hata kinachong’aa sana kikiachwa bila kutuzwa, ni suala la muda tu kitaharibika hata kupotea kabisa.

Hujawahi kusikia chuma kikilalamika kuwa ni nani amekiharibu kwa sababu kinajua ni chenyewe ndicho kilisababisha kuharibika kwake.

Kinachoharibu chuma ni kutu inayotengenezwa na kutanda chuma hicho. Lakini ili kutu ikipate chuma, ni lazima chuma hicho kikaribishe maji na hewa na kuungana na chuma hicho.

Kimojawapo kisipokuwepoa, kutu haitokei. Hivyo kama chuma kisiporuhusu maji yaanguke hapo, hakuna kutu itakayotokea na chuma hakitaharibiwa.

Rafiki yangu! Kitu cha kwanza kabisa kinachoharibu maisha yako ni mtazamo wako hasi. Mtazamo huu hasi ndiyo unakufanya kuchukua hatua zinazoharibu maisha yako.

Mtazamo hasi umejengeka kwa kuruhusu mawazo hasi yaingie ndani yako na kukaa humo. Haya yameamua vitendo hasi ulivyovichukua na matokeo hafifu au ya uharibifu uliyoyapata.

Yafuatayo ni mawazo hasi yaliyosababisha uharibifu kwenye maisha yako;

1. Siwezi. Kwa kusema huwezi umejiwekea ukomo wa kutoweka jithada zozote. Kwa kusema siwezi umechukua hatua ndogo zilizokupa matokeo madogo usiyoridhika

2.Wivu. Kwa kuwa na wivu mbaya umewachukia wale waliopiga hatua kubwa kuliko wewe. Umetamani wangeporomoka ili washuke na kulingana na wewe. Badala ya kuweka jitihada kujenga maisha yako unawawazia waliofanikiwa na kutaka wabomoke.

Jifunze kutoka kwa waliofanikiwa ili na wewe ufikie hatima yako njema.

3.Kuna njia ya mkato. Umeamini unaweza kufanikiwa kwa njia za mkato. Kila siku unaanzisha kitu kizuri lakini ukikutana na ugumu unaacha ukiamini kuna kitu kingine kitakupatia mafanikio kirahisi.

Rafiki haya mawazo yanaharibu muda, uzingativu, fedha na nguvu zako bure. Hakuna njia ya mkato. Chagua jambo moja kisha jitoe mzima mzima mpaka likupe mafanikio.

4. Utajiri ni mbaya. Kuna dhana hizi kuwa utajiri ni mbaya na watu matajiri ni wabaya, iwe umeikuza baada ya kushindwa au kabla, haya ni mawazo yaliyeta uharibifu mkubwa kwenye kipato chako.

Utajiri ni mzuri . Japo fedha sio vitu vyote lakini ni vitu vingi. Fedha inakupa uhuru mwingi.

Weka jitihada kupata fedha nyingi uwezavyo kisha uwe huru na uambukize uhuru huo kwa watu wengine.

Kwa kuwa umeyakaribisha mawazo haya, yametengeneza kutu na kuleta uharibifu maishani mwako.

Habari njema ni kuwa kama bado upo hai una nafasi ya kubadilisha mtazamo wako na kuanza kuleta matokeo mapya maishani mwako.

  1. Usiseme siwezi. Una nguvu kubwa ndani yako, jiulize nafanyaje?
  2. Acha wivu, usiwaombee waliofanikiwa waporomoke jifunze kwao ili na wewe upande kwako.
  3. Hakuna njia ya mkato. Chagua jambo moja. Jitoe likutoe
  4. Utajiri ni mzuri. Toa thamani kwa wengine nao watakulipa na kukupa utajiri.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *