Hiki Ndicho Kinachotokeo Unapoanza Na Kuendelea Kusoma Vitabu


Categories :



Kama unajua kusoma lakini husomi vitabu ni sawa tu na mtu asiyeweza kusoma.

Kama unapata muda wa kula halafu unasema huna muda wa kusoma hujitendei haki kwa kiwango kikubwa sana.

Kauli hizi mbili zitoshe kuonyesha ni kwa namna gani usomaji hasa wa vitabu ulivyo muhimu sana katika maisha yako.

Usomaji wa vitabu si utaratibu ambao umezoeleka sana kwa nchi nyingi za Kiafrika. Lakini inaweza kuwa miongoni mwa sababu kubwa zinazoleta utofauti wa maendeleo kati ya nchi zilizoendelea na zile zilizoendelea.

Leo nitakushirikisha sababu tano za kwa nini usome vitabu kama kweli unataka kufanikiwa maishani mwako;

1. Ni chakula cha akili. Kama vile mwili usipopata mlo kamili unavyodhofika ndivyo akili inavyodhofika usipoilisha maarifa sahihi.

Kadhalika kama mwili unavyoharibika kwa kuulisha sumu, ndivyo akili yako inavyoharibika unapolisha uchafu.

Lisha akili yako maarifa tena maarifa safi.

2. Ni kioo chako. Unavyofanya itakuwa sahihi hata kama unakosea mpaka pale utakapopata usahihi.

Kama vile unavyoweza kujiona uchafu pale unaposimama mbele ya kioo, vivo hivyo unavyoweza kujiona makosa yako unaposoma vitabu.

3. Vinakupa mbinu. Akili yako inazaliwa bila kitu, kuna maswali utayapata maishani ambayo huna majibu. Sehemu mojawapo sahihi ya kupata majibu ya maswali hayo ni kwenye vitabu. Una swali! Pata kitabu husika.

4. Hamasa. Safari ya mafanikio ni ngumu sana yenye vikwazo vingi hivyo kukupelekea kukata tamaa. Lakini kwa kusoma vitabu unakutana na watu waliopotia changamoto kama za kwako au zaidi na unahamasika na kuchukua hatua tena.

5. Kukua kwa haraka. Mafaniko yako ya nje yatatokana na mafaniko yako ya ndani. Kama tunataka ukue nje basi anza kukua ndani kwanza; fikra, imani, uvumilivu nk. Ukuaji huu wa ndani unaupata kwa kusoma vitabu.

Ndugu! Kuna vitu vingi ulivyojaribu na vingi havikukupatia matokeo sahihi. Nakushauri sasa ujaribu kuanza kusoma vitabu na kutumia maarifa, hakika utapiga hatua kubwa zaidi.

AMSHAUWEZO Consultants ina vitabu muhimu sana kwa ajili ya kutambua nguvu yako ya kipekee uliyonayo ndani mwako. Lakini pia ni vitabu vinavyokuongoza kuamsha uwezo huo kupiga hatua kubwa zaidi ya ulizofikia sasa. Vitabu vipi ungependa kuanza navyo? Chagua hapa;

1. AMSHA UWEZO WAKO HALISI
2. DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO
3. UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA
4. JENGA NIDHAMU KALI

Muda wa kupanda mti wa kivuli ulikuwa miaka 20 iliyopita lakini kama hukufanya hivyo muda mwingine sahihi ni sasa.

Usihuzunike kwa kuona kuwa umechelewa kuanza kusoma vitabu, huu pia ni muda sahihi kwako. Wasiliana nasi: 0752 206 899 tukuhudumie.

Anza Leo Anza Sasa Anza na Vitabu hivyo hapo juu.

Asante sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *