Huyu Ndiye Mtuhumiwa Wa Kwanza Wa Kushindwa Kwako. Mfunge Leo…
Kuna mambo mengi umefanya lakini umeishia kushindwa. Kuna muda mrefu umepita lakini huoni ukipiga hatua kubwa.
Umepanga mara nyingi kufanya vitu vikubwa lakini changamoto zipokuja ukaishia kukata tamaa.
Kila ukiwaona watu wamepiga hatua kubwa unawaonea wivu na kujilaumu kwa nini na wewe hujapendelewa kama wao!
Umekuwa ukiwatafuta watuhumiwa wa nani anayesababisha hali hii ya kushindwa kwako,pole kwa kumkosa. Lakini habari njema ni kuwa leo unafahamu mtuhumiwa wako wa kwanza na mkubwa wa kushindwa kwako.
Mtuhumiwa huyo hayupo mbali nawe bali ndani yako, naye ni FIKRA. Bahati mbaya huwezi kumshika kwa mikono.
Kila kitu unachokifanya kinaanza kama wazo. Hatua na matokeo unayoyapata yanaathiriwa kwanza na mawazo uliyoyatengeneza kwenye fikra zako.
Napoleon Hill alisema “What the mind of man can conceive and believe, it can achieve.” ikiwa na tafsiri kuwa chochote ambacho akili ya mtu itakipokea na kukiamini, basi itafanikiwa.
Hii ina maana kuwa yale uliyoshindwa kwenye maisha yako yametokana na yale ambayo fikra yako ilipokea na kuamini.
Kama kuna mabadiliko yanatakiwa kufanya ili kupata matokeo ya utofauti basi yanatakiwa yaanzie ndani mwako, yaani kwenye fikra zako.
Kinyume cha kushindwa ni kufanikiwa kama matokeo ya kushindwa yamesababisha na fikra ulizokuwa nazo, hii inamaanisha kuwa ili kuweza kupata mafanikio unatakiwa kubadili uelekeo wa fikra zako kwanza.
Fikra gani zimekufikisha kwenye kushindwa au kupata matokeo madogo yasiyokuridhisha? Je mabadiliko gani uyafanye ili uanze kupata matokeo unayostahili?
Usiwe na wasiwasi juu ya hilo. AMSHAUWEZO Consultant tumekuandalia semina iliyobebwa na kichwa PIGA U-TURN 101 ZA MAISHA YAKO. Kupitia semina hii utatambua fikra zote zilizokuwa zinakupoteza kisha kupiga U TURN na kwenda uelekeo wa fikra sahihi.
Kupitia semina hii utamtambua vizuri huyo mtuhumiwa wa kwanza wa kushindwa kwako na kumfunga kabisa.
Habari njema ni kuwa mpaka mwisho wa semina utakuwa umetambua hatua 101 ulizokuwa unazikosea na hivyo kuwa na hatua 101 zilizosahihi za kukufanya kuisha maeneo 10 ya maisha yako kama; binafsi, fikra, kazi, fedha/utajiri, biashara, nidhamu,…..kwa mafanikio makubwa.
Semina hii itafanyika kuanzia Julai 20 – 29, 2023 kwa njia ya kundi maalumu la wasap.
Ada ya semina hii ni sh 10,000/ unayolipia kupitia MPESA; 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Pata picha unapata hatua sahihi 101 za kubadili uelekeo wa maisha yako, lazima upige hatua kubwa sana.
Ili kujihakikishia nafasi hii nakushauri ujiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hiki; https://chat.whatsapp.com/Lmel6ehEr30K5a1S1BCEYu
Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na;
Mwl. Alfred Mwanyika
0752 206 899
www.amshauwezo.co.tz
Karibu sana.